Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

 


CNN
TBN
BBC
Times
Islamtz.org
Winners
Maranatha
Intergrity

China Today

Japan Times

Korea Online

China Site

China Maps

USA Today

Google Seach

China English

Gv China

China view

China news

China
Natinal
News

China Tech

India News

India Times

India Daily

Gospel of
Jesus

USA Gospel

Gospel
Church

Dubai news

Africa News

Gospel Music

US VISSA

BBC
Bush
Curches
Gospeltv
munishi
Mkapa
usgospel
Times
GTV
GTVGOSPEL
Jesus
God
Faith
Life
Kenya
Tanzania
Uganda
Africa
Japan
Toyota
China
Korea
India
Nation
News
Online
Nyerere
Kibaki
Museveni
Mugabe
KOFFI ANNAN
Nairobi
Dar
Goverments

gospel TV

gospelradio

Gospel radio

gospelnews

Gospel news


GOSPEL
GTV.COM


TV ya INJILI
Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM

Tel. 254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com


The lives of 33 people were cruelly snuffed out in a single night, 27 of them killed by police battling Mungiki suspects in a swoop triggered by the murder of two security officers on patrol in the sprawling Mathare slums in Nairobi. (Reply) Munishi2 (2 days ago) marked as spam "Police were beating anyone they came across in this area. It was terror like I have never seen before. I was injured on the leg," said Joseph Njoroge, a resident, pointing at a deep cut. crackdown was a reaction to the killing of police constables John Matinde and Philip Lengai, who appeared to have either run into an ambush or were simply random victims of members of the sect. Sect adherents are believed to roam the sprawling Nairobi slums, collecting protection fees.


Kubaka wanawake na kupora pesa na simu za mikononi, ndio uliokuwa mtindo wa GSU waliotumwa MATHARE kuwasaka wauaji waliowaua Polisi wawili na kumjeruhi mmoja. Hatuungi mkono kuuawa kwa polisi hao, lakini kuua watu 33 kama kulipiza kisasi, inatisha. (Reply) Munishi2 (2 days ago) marked as spam Kwanza tutajuaje kwamba waliouawa ni wahalifu? Je MATHARE hawakai raia wema ambao hawajuhusishi na vitendo viovu? Au kuwa masikini Kenya ni hatia? Kama ni hatia kwa nini masikini hao wasifikishwe mahakamani kujibu kwa nini wao ni masikini? Kuwaua kutamaliza tatizo?

Wahalifu wanapofanikiwa kuifanya serikali ihalifu, ushindi unabaki na wahalifu. (Reply) Munishi2 (1 day ago) marked as spam Nani aiamshe serikali kutoka usingizi mzito? Walipoingia madarakani walianza kuithibiti sekta ya matatu. Sekta hiyo ndiyo iliyokuwa ikiwatunza Mungiki kwa makubaliano au bila makubaliano na hakuna aliyewkuwa akiuawa. Serikali ilipoingia kichwa kichwa na bila kujali waliokuwa wanatunzwa na sekta hiyo watakula wapi, iliharamisha shughuli zao hizo.

Serikali inayojali maslahi ya matajiri wachache, inaonekana kushindwa kuhimili mafuriko yanayosababishwa na masikini walio wengi. Hakuna suluhu bila kupambana kwanza na umasikini. Unapowatuma Polisi ambao nao hawajashiba, badala ya kupambana na uhalifu, watatumia njia hiyo kuwapora wananchi ambao nao ni masikini. (Reply) Munishi2 (1 day ago) marked as spam Polisi masikini wanapowapora raia masikini mali zao, lawama zinairudia serikali iliyoshindwa kuumaliza umasikini katika raia wake.Hakuna anayeruhusiwa kuua kwa sababu yeyote. Serikali inapowaiga wahalifu na kuamua kufanya mauaji, Yenyewe inakuwa mhalifu namba moja.

Je hata hawa watoto wa shule ni MUNGIKI? Kwamba imekuwa ilivyokuwa, serikali haiwezi kukwepa lawama. Wananchi masikini hawawezi kuiondolea serikali matajiri inaowalinda na kuwategemea, lakini serikali inaweza kuwaondolea wananchi umasikini. Tatizo la MUNGIKI ni la kisiasa siyo la kijeshi. Kulitatua kijeshi ni kuongeza mafuta ya petroli kwenye moto unaowaka.

Wengine wanaliona tatizo hili kama ni mbinu ya serikali kuwatia raia hofu hasa tunapoelekea uchaguzi mkuu. Kuna wale wanaosema Kibaki anahisi atashindwa uchaguzi na anatengeneza mazingira ya kumuwezesha kufanya lolote kubaki madarakani. Tena kuna wale wanaoelekeza vidole vya lawama kwa vyama vya upinzani. Wanasema wanawatumia Mungiki kuikejeli serikali kwamba imeshindwa majukumu yake ya kuwalinda raia na mali zao. Je wewe unalionaje sakata hili?

Inawezekana serikali ishindwe kumaliza kundi au makundi ya uhalifu nchini? Ikiwa jibu ni ndiyo itakuwaje serikali hiyo itakapovamiwa na maadui wa nje? Kibaki ndiye aliyewatengenezea SOMALI serikali na kuwapa usafiri mpaka Somalia. Na hivi karibuni anatarajiwa kutengeneza serikali nyingine ya Tanzania chini ya Rais Munishi na aisafirishe kupitia Namanga mpaka Dar. Je atashindwa kumaliza kundi la mungiki bila kuwaua? Ninaamini anaweza.

GTV tunamtaka Rais wa Kenya atumie hekima na uangalifu mkubwa katika kulitatua tatizo hili. Kiongozi mzuri siyo yule anaekimbilia njia za mkato ambazo hazimalizi tatizo, bali ni yule anayetumia muda kufikiri jinsi atakavyolitafutia tatizo uvumbuzi wa kudumu. Kibaki akitumia hekima ya hali ya juu ataliweza hilo.

Usiongeze majeneza, bali wabadilishe wauaji wawe raia wema. Ikikushinda tumia wakuu wa dini. Hiyo ndiyo kazi yao. Kuwabadili wale serikali na mtutu wa bunduki imeshindwa kuwabadili.

Kwamba wazo la Mungiki limemwaga damu za Wakenya, lazima watu wote wanaofikiri waanze kulichambua wazo lenyewe. Afrika hatuendelei kwa sababu ya kuyaogopa mawazo mapya.Serikali hutumia mamilioni ya pesa kuangamiza mawazo badala ya kuyaendeleza na kuyafanyia kazi. Tuseme Mungiki ni wezi. Japo hatuna hakika. Sasa Mwizi akikuambia naiba kwa sababu mimi ni masikini. Mkinipa kwa mwezi shilinhgi 100 za Kenya kila nyumba, nitawalinda msiibiwe. Au nitaacha kuwaibia. Na waliokubali kufanya hivyo ikawa kweli mali zao hazikuibwa. Je hilo ni wazo tata? Kulikuwa na haja gani ya serikali kuliharamisha wazo hilo?

Utaniambia Mungiki ni mkusanyiko wa mawazo mengi mabaya. Sawa. Kwa nini tusiyachukue mawazo yao mazuri na yale mabaya tuwarekebishe waache? Hakuna mwanadamu tupu bila mchango kwa jamii. Tatizo ni wanasiasa wachache wanaofikiri kwamba mawazo yao tu ndiyo yanayoweza kuwaongoza wengine. Kama serikali pamoja na majeshi yote hawajaweza kumaliza uhalifu nchini sioni kwa nini wasisaidiwe na mawazo toka Mungiki japo wamewaharamisha. Kama ni kweli Mungiki waliweza kuleta amani Mathare kwa nini serikali wasiwatumie? Kama watu wachache ndani ya serikali wamefanya uhalifu, haina maana tutaiharamisha serikali kwa kufanya uovu ule ule.

Ndivyo Serikali ya Kenya inavyofanya katika kupambana na Mungiki.Wanasema wanaua, na wao watauawa. Sawa. Lakini mbona wanaouawa ni raia ambao hawajui hata Mungiki ni nini? Wazo likishafikia hatua ya kumwagika damu, halifutiki. Badala yake damu inaliandika kwenye bongo za watu wengi kwa mara moja. Kwangu naona serikali inatengeneza Mungiki wengi kuliko mwanzo. Kumaliza tatizo hili, ni kwanza serikali ipambane na uhalifu na wahalifu na siyo na Mungiki. Huwezi kupambana na wazo ambalo hujui kama hata wewe mwenyewe unaliamini. Ndiyo maana nataka sana kumjua mwanzilishi wa wazo la Mungiki. Wakati wazo lake linamwaga damu, na linawafanya wakuu wa serikali ya Kibaki kujikuna kichwa, Tena limeingia kwenye vyombo habari ulimwenguni, Hakuna wakati mzuri wa kulitetea wazo hilo kama sasa.

Vyombo vya habari nchini Kenya vinaonekana kugawanyika kuhusiana na Mungiki. Wakati wengine wanaiunga mkono serikali iwaangamize Mungiki, Hawajui mbinu gani itumike. Mbaya zaidi ni kwamba hata wanamedia wengine ni Mungiki. Wazo lililofikia wakati wake, ni kali kuliko makombora yote duniani. Huwezi kulimaliza kwa bunduki.Waafrika walipowaza UHURU wakoloni walishindwa kuzima wazo hilo. Kama masikini wa Kenya wanahisi kwamba serikali haiwajali, na wamewaza kujikomboa, mtakosea sana kufikiri majeshi ya Kenya yataweza kuwanyamazisha. Kupambana na wazo ni sawa na kuufukuza upepo. Leo ni Mungiki. Kesho akija mtu atoe wazo kwamba TV zote Kenya zifungwe kama haziwezi kuandaa vipindi, mtapambana naye kwa bunduki. Mnaruhusu TV ziwamwagie mawazo ya nchi za magharibi kiasi kwamba mzalendo wa Kenya akija na wazo la kuwasaidia Wakenya mnapambana naye kwa makombora. Mbaya zaidi hakuna wazo mbadala.

Kile nikionacho ni mbinu ya Mungiki ikitumika kila mahali. Wanahabari wanawatoza watu fulani pesa ili habari za watu hao zitawale vyombo vya habari. Je hiyo siyo mbinu ya Mungiki? Wanaposema wamalizwe, ina maana ili wao waendelee? Polisi huweka vizuizi barabarani, na kila MATATU huacha shilingi mia kila inapopita. Malori ya mchanga nayo huacha kiasi fulani cha pesa. Hapo haijalishi kama gari husika imetimiza sheria za barabara au la. Je wanapopambana na Mungiki ina maana wao wabaki wakikusanya pesa? Waalimu hukusanya pesa kwa wazazi ili watoto wafundishwe masomo ya ziada kuwafanya washinde mitihani. Wazazi wanaokataa kulipa watoto wao hubaguliwa na kuonekana kama watoto daraja la pili shuleni. Je huo sio UMUNGIKI? Redio za FM Kenya hucheza nyimbo za wasanii wale waliolipa kitu kidogo. Usipolipa hata kama nyimbo yako hutoa nyoka pangoni haichezwi. Ndiyo maana kila kukicha tunasikia nyimbo ambazo masikio hayataki, lakini yanalazimishiwa kusikia. Je watasema wao siyo Mungiki? Magereza wafungwa wenye pesa hukaa kama wako uraiani. Wale wasio na kitu lazima wapambane na ugali na maharage yasiyoiva. Je huo siyo UMUNGIKI? Kwa nini mnapambana na wazo ambalo wenyewe mnalifanya kwa siri? Je kosa la Mungiki ni kufanya wazo hilo hadharani?

Serikali ambayo ndiyo inayotunga sheria, ilisikika ikiwakemea mahakimu kwa kuwaachia huru watuhumiwa wa Mungiki. Yaani serikali ilitegemea kwamba mahakama zitawafunga watuhumiwa wote miaka mia gerezani hata kama hakuna ushahidi wa kutosha. Ikiwa serikali yenyewe haiamini katika sheria, tofauti yao na hao inaowaita Mungiki ni gani? Rais Kibaki mwenyewe alisikika akisema kwamba serikali yake haitawahurumia Mungiki. Wakikamatwa watauawa. Hakusema sheria itachukua mkondo wake, bali alisema 'Utauawa weweeee!!! ' Unafiki mkubwa huu. Lazima tuukomeshe. Halafu waziri wake wa ulinzi alisemaje?' Hata wale tuliowakamata, siwezi kuwaambia wako wapi. Bali mtasikia mazishi ya fulani ni kesho.'

Usishangae kuwaona polisi wakiwaburuza watu kwa jazba na nguvu kupita kiasi, ni amri kutoka juu. Kwanza kwa rais mwenyewe, halafu kutoka kwa waziri wa ulinzi, kisha kutoka kwa mkuu wa Polisi, halafu uteremke kwa sajenti au kopro, halafu kwa hawa makurutu unaowaona wakikanyaga watu bila woga, wengine wanacheka mbwa anapomvua mwanaume suruale na kadhalika. Polisi wakipewa baraka nyingi hivyo wanaweza kufanya lolote. Kwanza wana baraka ya rais, Pili wana baraka ya waziri wa ulinzi, tatu wana baraka ya mkuu wa polisi, Nne wana baraka ya vyombo vya habari ambavyo karibu vyote vinaunga mkono kumalizwa kwa Mungiki. GTV tunauliza hivi. Mungiki ni wazo tata? Kwa nini serikali inaliogopa wazo hilo? Serikali iliharamisha wazo, au vitendo vya uhalifu? Mungiki ambao hawajajihusisha na uhalifu watauawa? Je serikali ina mbinu gani kujua kwamba vijana wote ni Mungiki? GTV tunapinga uhalifu hata kama utakuwa umefanywa na serikali iliyo madarakani. Hatuwezi kupinga uhalifu wa serikali tuunge mkono uhalifu wa yeyote. Awe ni ODM au KANU, Mungiki au NARC KENYA.







 
| http://munishi.com |