Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

 


CNN
TBN
BBC
Times
Islamtz.org
Winners
Maranatha
Intergrity

China Today

Japan Times

Korea Online

China Site

China Maps

USA Today

Google Seach

China English

Gv China

China view

China news

China
Natinal
News

China Tech

India News

India Times

India Daily

Gospel of
Jesus

USA Gospel

Gospel
Church

Dubai news

Africa News

Gospel Music

US VISSA

BBC
Bush
Curches
Gospeltv
munishi
Mkapa
usgospel
Times
GTV
GTVGOSPEL
Jesus
God
Faith
Life
Kenya
Tanzania
Uganda
Africa
Japan
Toyota
China
Korea
India
Nation
News
Online
Nyerere
Kibaki
Museveni
Mugabe
KOFFI ANNAN
Nairobi
Dar
Goverments

gospel TV

gospelradio

Gospel radio

gospelnews

Gospel news


GOSPELGTV.COM


TV ya INJILI
Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM

Tel. 254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com

Machozi ya Uhuru


Kiongozi wa Upinzani Kenya Bwana Uhuru Kenyata akilia machozi ya Uhuru
Tatizo la wachuuzi halitafutiwi dawa makusudi. Wanasiasa huwatumia wachuuzi wakati wa uchaguzi.Wengi wa wapiga kura katika nchi za Afrika ni masikini wanaojitafutia riziki kwa njia za kuchuuza biashara ndogondogo. Siyo dhambi kufanya hivyo. Wafanyibiashara wakubwa huanza kwa kuchuuza kwanza. Kwamba wanasiasa watawaamuru polisi wawamiminie wachuuzi risasi za moto vichwani, hilo linatisha. Sambamba na hilo, hatuungi mkono hatua ya wachuuzi kulipiza kisasi kwa kumuua askari polisi. Wote wamekuwa wauaji. Lakini haiingii akilini kuona polisi wa kenya wakiwaua raia wa Kenya kwa kosa la kujitafutia riziki zao za kila siku. Hata kama Nairobi inatakiwa kuwa safi, lazima usafi huo uwe wa kiwango cha nchi changa za kiafrika ambazo umasikini uko kwa kiwango cha kutisha. Kuigiza usafi wa miji ya nchi zilizoendelea, kutaigawa nchi katika matabaka ya matajiri wachache wasiotaka kuona masikini karibu nao. Tunaomba isifikie mahali pa kutungwa sheria inayosema kuwa masikini ni kosa linalopaswa kuadhibiwa kwa kupigwa risasi kichwani au kifuani.Tunasikia wachuuzi waliouawa walipigwa risasi kichwani na kifuani. Wale wanaoitwa Majambazi sugu pia hufa kwa mtindo huo.Tofauti ya mtu anayejitafutia kihalali na majambazi iko wapi? Na serikali ya Kibaki inategemea kuchaguliwa tena? Basi waonyeshe moyo wa kuwajali masikini, na walitafutie suluhisho la kudumu suala la wachuuzi. Hatutarajii kuona picha kama hizi katika Kenya huru. Na ni kwa nini Uhuru Kenyata analia? Je Machozi ya Uhuru yanaashiria kwamba uhuru kamili ni bado? Kama alienda kuwatuliza wachuuzi mbona polisi waamue kuutawanya umati kwa kuwatupia mabomu ya machozi? Hawakujua Uhuru alikuwa amekuja kuwaombea wachuuzi uhuru wa kufanya biashara katika nchi yao? Au waliona kura zikibadili mkondop kuelekea kwa kiongozi wa upinzani? Je waliyoyafanya tatabadili chochote? 2007 siyo mbali tunasubiri tuone.

Oh siyo kasheshe jingine tena!!

Mabaki ya Kanisa la Redeemed baada ya kubomolewa na wale walioitwa askari wa jiji usiku wa manane

Tukifikiri yataishia hapo, sasa serikali imeanza kuyabomoa makanisa yaliyopata viwanja wakati wa serikali ya Moi. Sehemu za kuabudia Kenya hupewa makanisa yanayoonekana kuiunga mkono serikali.Wakati wa Moi, serikali yake iliungwa mkono na kanisa la Redeemed Gospel, kiasi kwamba Bishop Kitonga angeweza hata kujenga kanisa huko ikulu bila kuzuiwa na yeyote. Ni katika mazingara hayo kanisa hilo liliweza kupata kibali cha kujenga kanisa Uhuru Pack, sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kiwanja cha kujipumzisha. Serikali mpa imeona hiyo haikuwa sawa na wakawapa barua ya kuhama hapo ifikapo tarehe 6 mwezi wa sita. Tarehe hiyo ilifika na kanisa bado likawepo. Serikali wakaamua kufanya KIKOMANDOO. Usiku saa sita wakaanza kulibomoa kanisa hilo.Mchungaji badala aombe Mungu, akakimbilia kwa mwanasiasa ili amsaidie kulinda kanisa lisibomolewe. Vidole havitoshani, na wanasiasa hawatoshani kiuwezo. Ikawa amri ya kubomoa ilitoka juu zaidi ya mwanasiasa aliyekuja kuzuia ubomoaji. Wanasema ni askari wa jiji, lakini mimi siamini kwamba askari hao wana uwezo wa kuwazidi nguvu walinzi wa waziri na kuweza kuwanyanganya silaha kisha kuwapa kipigo cha mbwa mwizi waziri na walinzi wake. Wengi wanaamini kwamba kazi hiyo ilitekelezwa na makomandoo sawa na wale walioivamia KTN na Standard.Masaa walioamua kufanya zoezi hilo ndiyo yanayowapa mashaka wengi katika jamii ya wakristo.Hawajui ni kanisa gani litakalofuatia. Pastor James Maina Nganga naye yuko jirani tu na kanisa lililobomolewa, lakini yeye ametambua siri. Yeye husema wazi kwamba anaipigia debe serikali ya Kibaki. Ukiingia ofisini kwake, macho yako yatakutana na picha ya mchungaji huyo akisalimiana na Kibaki. Hakuna kosa kufanya hivyo, lakini swali wengi tunalojiuliza ni je serikali hii isiporudi madarakani kanisa hilo litasimama wakati wa serikali nyingine? Sisi GTV hatuna tatizo na makanisa kuunga au kutounga serikali mkono. Tunachosema ni kwamba haki ya kanisa kupewa kiwanja cha kujenga nyumba ya ibada isiingiliwe kisiasa.Hatutaki kuona kila serikali mpya ikibomoa makanisa ya serikali zilizotangulia. Na wachungaji waache kuwaabudu wanasiasa badala ya Mungu.

Hatimaye Mchungaji Joshua Mogera wa City Victory Temple kanisa lililobomolewa, ametambua kwamba msaada wake unatoka juu kwa Mungu na siyo kwa wanasiasa. Baada ya kanisa kubomolewa, sasa ameamua kumuomba Mungu amsaidie apate sehemu nyingine ya kuabudia. GTV tunanaungana naye katika hilo na tunamshauri safari hii aache kuwatumia wanasiasa. Ikiwezekana wanunue ploti na waanze kujenga jengo la kuabudia.



Warusi Artur Margaryan na Artur Sagarsyan, Waliozua Kasheshe Kenya


Kibaki Aguswa mahali
Polisi walipowaua wachuuzi watatu na wachuuzi kulipiza kisasi kwa kumuua Polisi mmoja, wengi walisubiri kwa hamu tamko kutoka kwa Rais wa Kenya mheshimiwa Mwai Kibaki Lakini rais alikaa kimya kana kwamba siyo jambo la ajabu. Ikaja ya pili. Waziri wake Profesa Kibwana alipatiwa kipigo cha mbwa mwizi pale alipojaribu kuwazuia makomandoo wasibomoe kanisa usiku wa manane. Walinzi wake walinyanganywa silaha na kupatiwa mkong'oto wa aina yake. Hapo pia Kibaki kama kawaida yake alikuwa kimya kama maji mtungini. Ukimya wa Kibaki unawashangaza hata waandishi wa habari ambao hawajui waguse wapi huyu mzee aongee. Tangu aingie madarakani sijawahi kumuona Kibaki akihojiana na waandishi wa habari. Lakini Gazeti la Nation na NTV wamejua wapi mzee huyu huguswa akaruka mithili ya mtu aliyegusa waya za umeme tena zenye moto.Kwa sababu GTV bado hatuna masafa ya kurushia matangazo yetu Kenya hatutathubutu kumgusa Mzee Kibaki hapo alipoguswa na Nation, Lakini tutawaonyesha story iliyomfanya Kibaki aicharukie Nation kama nyuki.


Duniani ni mahali pazuri sana kuishi. Kwani kadiri unavyoishi ndivyo unavyoona na kusikia mengi. Nani alijua siku moja gazeti la Nation lingeweza kuandika chochote kinyume na Serikali ya Kibaki? Wakati anaingia madarakani Nation liligeuka kuwa gazeti la chama na Serikali. Kwamba leo wamegeuka, ni wale wanaoishi tu ndio wana nafasi ya kuona na kusikia hayo. Pia ni nani angeweza kufikiri kwamba siku moja Rais mstaafu Moi angeweza kumsifu Kibaki kwa kukataa kuheshimu makubaliano ya awali yaani MoU? Ni mpaka uishi kwingi uone na kusikia mengi. Yaani uone na usikie watu wakikana watoto na mama waliyepata naye watoto hao, Kisha usikie watu wakijisifu kwamba wao ni waume wa mke mmoja wakifikiri inawaongezea heshima zaidi, Usiniulize walidanganywa na nani kwamba waafrika kuwa na wake wengi ni kosa? Hapo sina jibu. Tena usiniulize kama walio na mke mmoja huwa naye kinadharia huku wakiwa na vimada kila kona? Hapo jibu pia unalo mwenyewe.Ombi la GTV kwa Kibaki ni hili. Mzee tusaidie utuwekee milingoti ya kurusha matangazo ya TV hata kama ni Nairobi tu, nasi tutakusaidia kujibu mashambulizi kama haya yanayotoka Nation. Tunamaanisha, na tunashukuru kimbele.


Gharama ya kuwa na gari Nairobi

Siku hizi ukifanya kosa barabarani, utakutana na hawa jamaa. Watakupiga, halafu wataamua wakushitaki kwa kosa gani, na kisha upelekwe mahakamani kama hutaongea lugha wanayoijua. Kabla uamue kununua gari Nairobi, Siyo vibaya ukajifahamisha unatakiwa kuilipia kiasi gani kwa siku. Kwanza kupata mahali pa kuliegesha lazima umlipe atakayekuonyesha mahali hapo KSHS 30 na kuendelea. Kisha askari wa tume ya jiji naye utamlipa KSHS 70 kila siku na ninasikia gharama hiyo itaongezeka kufikia KSHS 200 kwa siku. Ukifikiri umemaliuza kulipa, bado unatakiwa ulipe KSHS 50 na kuendelea kwa mlinzi atakayekulindia taa za gari lako pamoja na vibandiko vinavyoonyesha gari yako ni aina gani zisingolewe. Ukipuuzia, yeye huyo huyo ndiye atakayefanya mpango gari yako iwe haina vibandiko kwenye magurudumu, au taa za kuonyeshea ishara utazikuta hazipo. Ukifikiri yataishia hapo, kuna yule atakaekuombea nafasi kwa wenye magari wakupe nafasi ya kutoka ulipoliegesha gari lako. Huyo hupokea chochote. Sasa unaweza kuelekea nyumbani, na ni kama hukufanya kosa lolote la trafiki ukamatwe. Kama utakuwa umekamatwa basi kiwango unachotakiwa kubeba kwa siku siyo chini ya KSHS 20,000 ili uwe salama pande zote. Ukikosa kiwango hicho, usishangae siku moja utakosa kurudi nyumbani, na watakapokutafuta hospitalini wakukose, tena wakutafute chumba cha maiti wakukose, basi wakienda jela watakukuta umefungwa miezi miwili au mitatu kwa kosa la wewe kuwa na gari bila kubeba KSHS 20,000 kila siku kukufanya uwe salama. Na hapo ni kama hujagonga Benzi ya mtu nyuma uvunje taa moja tu ya nyuma. Kama gari yako ni kama yangu, basi itauzwa, na bado haitatosha kuilipa taa moja ya Benz.

Baada ya kisa cha Artur Margaryan, Serikali imeonyesha kuviimarisha vyombo vyake vya usalama ili vionekane kwamba vinafanya kazi ipasavyo. Lakini rushwa bado ni kikwazo kikubwa. Pesa zinazungumza sauti kubwa kuliko Haki. Huwezi kujua mizizi ya rushwa imeota kiasi gani, hadi ukutane na ule unaoitwa mkono wa sheria. Hapo ndipo utakapokutana na watu walio tayari kukudhalilisha kwa kiwango chochote mpaka useme mwenyewe ni bei gani nitoke hapa? Watakusukuma kushoto kulia, watakutusi na mwisho watarudia rudia kukufahamisha kwamba kesi yako faini yake ni kiasi kadhaa, au ufungwe miezi kadhaa, na mwisho watakuambia ukitoa rushwa kiasi fulani utatolewa. Ningesimuliwa haya ningekataa, lakini yalinikuta mwenyewe. Ilikuwa tarehe 20 mwezi wa sita mwaka 2006. Nilikuwa nimetokea Mombasa na nikashika Ngong Road kuelekea Ngong. Kabla nifike makao makuu ya usalama barabarani, kuna barabara ya 'ONE WAY' Lakini magari yanapita mawili. Ya mkono wa kulia inaishia mahali bila taarifa, na ni lazima uifuate kurudi ulikotoka au uombe nafasi ya kurudi kwenye 'LANE' ya kushoto uendelee na safari ya kwenda Ngong. Nikiwa katika kuomba nafasi ya kurudi kushoto, alitokea mwana usalama barabarani aliyekuwa amejificha mbele kidogo akingojea windo la siku hiyo.

Aliniamuru nifungue mlango aingine ndani ya gari langu, na tuliandamana hadi makao makuu ya usalama barabarani ambako walizuia gari pamoja na mimi. Nilipotaka kujua kosa langu, waliniambia ni kuyapita magari mengine kihatari. Nywele zilinisimama nikijua kwamba sikuwa nikifanya hivyo. Kila nilipojaribu kujieleza, ndivyo nilivyozidi kusukumwa niingie ndani ya 'sell'. Hakuna aliyenisikiliza hata wale niliodhani kwamba wananifahamu. Nikakumbuka msemo kwamba usiwahi kuwa rafiki wa askari polisi. Ikibidi hata mke na watoto wake anaweza kuwakamata ili aongezewe cheo. Ilikuwa saa tatu asubuhi, na tuliwekwa hapo mpaka saa nane tulipopelekwa mahakamani. Pamoja nami kulikuwepo madereva wa MATATU pamoja na makondakta wao, bila kusahau mzee mmoja wa asili ya kiasia ambaye maaskari walikuwa wakimwita 'mhindi' Kwao ilikuwa ni kama sherehe kuwa na mhindi anayepelekwa mahakamani kna kwamba haikuwa kawaida yao. Hata ofisa msimamizi wa kituo ambaye ni Mkikuyu alisikika mara kwa mara akiuliza kama bado yule mhindi yuko katika msafara wa watu wanaopelekwa mahakamani.Tangu Kibaki ashike madaraka wakikuyu wamewekwa sehemu muhimu hasa polisi na mahakamani. Nasikia ni kila mahali, lakini mimi nimeshuhudia hilo Polisi na mahakamani.

Baada ya kuhukumiwa nililipa faini ya KSHS 2000 na kuachiliwa huru. Lakini baada ya masaa saba ya kusukumwa kushoto kulia na pingu mkononi.

Tulipofikishwa mahakamani ndipo tulipoanza kusikia kila mtu akitajiwa kosa lake na faini yake, na kiwango anachopaswa kulipa kama rushwa ili ajinunulie uhuru. Kosa langu niliambiwa adhabu yake ni faini ya shilingi 6000 pesa za Kenya, au nitoe elfu mbili na mia tano niachiwe bila kufikishwa mahakamani. Niliamua liwalo naliwe. Sitatoa rushwa. Baada ya wenzetu kukubali kununua uhuru wao, waliitwa na hatukuwaona tena. Tuliingizwa kwenye seli ya kungojea kwenda mahakamani, na hapo askari jela alitufokea kwa sauti yake yote. "Ingieni si mmeamua kuja huku?" Muda wote huo tulikuwa tusisukumwa kushoto kulia, ili ikiwezekana tufanye kile walichokitaka. Mioyo yetu ilivyozidi kuwa migumu ndivyo mateso na matisho yalivyozidishwa. Pingu zililetwa na tukafungwa pingu wawili wawili.

Tulianza safari ya kwenda mahakamani tukilindwa na askari zaidi ya kumi. Nafikiri hata Artur mMargaryani wasingewekewa ulinzi mkali hivyo. Ikaja zamu ya kuzunguka mahakama yote tukielekea kwenye mahakama ya makosa ya usalama trafiki. Tulipoingia tulifunguliwa pingu na kungoja zamu ya kuitwa na kuhukumiwa. Tulionywa kwamba tuwe wasikivu na tutoe sauti kubwa tunapokubali au kukataa kosa. Majina yalipoanza kuitwa, ndipo nilipogundua kwamba wengi waliokuwa wameshitakiwa siku hiyo walikuwa Wakikuyu. Kama ulikuwa umedanganyika ufikiri kwamba Kibaki kuweka Wakikuyu kila kona alikuwa na lengo la kuyanyanyasa makabila yale mengine, basi itakubidi ufikiri upya. Yale niliyoyaona mahakamani ni sawa na Wakikuyu wakikulana wenyewe. Wengi walikuwa wameshitakiwa makosa ya kuendesha magari bila vithibiti mwendo. Wengi walikubali makosa yao huku wakionyesha risiti za vithibiti mwendo, na kudai kwamba magari yao yamewekwa vifaa hivyo lakini askari wameamua makusudi kuwashitaki kwa makosa hayo ya uongo.

Jaji alipowauliza kwa nini wanakubali huku wakijua wazi kwamba wameshitakiwa isivyo halali? Majibu karibu yote yalifanana. Walisema ni rahisi kukubali na kulipa faini ya Ksh. 8000 kuliko kusubiri kesi ndefu ambayo hawajui itaisha lini, na mbaya zaidi gharama ya kutetea haki ni kubwa zaidi kuliko faini wanayolipa. Ilipofika zamu yangu, tayari nilijua cha kufanya. Nilikubali kosa, na kwa bahati nikalipishwa faini ya KSHS 2000 tu. Kwangu nilisikia kufarijika kwani ningetoa rushwa ningekuwa nimetoa nyingi kuliko hizo, na kisha roho yangu ingeumia kwani nimetoa rushwa. Kama faraja yangu inamaanisha chochote kwako ni sawa. Kuna wengine wanaosema kwamba zote ni rushwa tu. Serikali inapoamua kutengeneza sheria kwa lengo la kupunguza ajali barabarani na kuongeza ajali hizo kwenye mifuko ya wananchi wake, haiwasaidii wananchi husika.

Hatujui ni kwa kiwango gani sheria za Michuki zimepunguza ajali barabarani, lakini kuna jambo moja ambalo halipingiki. Sheria hizo zimewaongezea uwezo askari wa usalama barabarani na sasa wananchi lazima wacheze mikononi mwao. Hata sura zao zinaonyesha kwamba wanaoifaidi biashara ya Matatu ni maaskari wa barabarani kuliko wanaozimiliki matatu zenyewe. Kuna wengine wanasema kwamba siku hizi serikali imehamisha pesa kutoka kwa wenye matatu na kuzihamishia mifukoni wa wana usalama barabarani. Maisha yao yalibadilika ghafla tangu Kibaki aingie madarakani. Kitambo walijulikana kwa kupokea rushwa kuanzia KSHs 20, sasa nasikia hata mia mbili hawachukui. Bei ya RUSHWA imepanda kuanzia shilingi 1000. Wana matatu wanasema siku hizi askari ndiye anayeamua kosa gani akushitaki nalo. Wanajua magari hayakosi makosa. Wakikushika na uongee nao vizuri, wanakuambia utoe sare ya kazi ili ushitakiwe kwa kutovaa sare, nafaini yake ni KSHS1000. Au akikuhurumia sana, atakushitaki kwa kutofunga mkanda, na faini yake ni KSHS 500. Usisahau abiria nao wamo kwenye sakata hilo, jambo linalowaongezea askari mawindo yao. Baada ya hayo yote kufanyika, bado serikali ya Kibaki itawaomba wananchi kura mwaka 2007. Pengine watachaguliwa. Huwezi kujua. Tusubiri tuone.Ni Ukweli kwamba sasa polisi wa usalama barabarani wanakula kuku kwa mrija. Yaani wao ukiwauliza serikali gani iliyowafungulia mifereji ya pesa kumwagika kwao, watakujibu ni serikali ya Narck. Tena watasema Kibaki aitawale Kenya milele. Lakini kwa wananchi wa kawaida sitoshangaa jibu likawa tofauti.


Ukifikiri ni wanaume tu walioshitakiwa kwa makosa ya Trafiki utakosea. Hata wanawake walikuwepo kwa mamia na kosa lao ni kutokufunga mikanda wanaposafiri na MATATU. Wengi huona uchafu ndani ya mikanda hiyo kama kero na huamua kusafiri bila kuchafua nguo zao. Kwa hiyo ukiwa unatumia Usafiri wa Matatu kuwa macho na ubebe pesa za ziada endapo utakutana nao. Watafikiri umechelewa kazini kumbe uko jela.

Kinachoumiza roho ni jinsi serikali inavyowanyanyasa wamiliki wa MATATU kiasi cha kutufanya wengine tuamini kwamba kufanya biashara ya MATATU Kenya ni haramu. Kuna wanaosema Serikali Ya Kibaki ni kama suala pekee waliloingia madarakani kufanya ni kuwanyanyasa watu wa MATATU. Kuna Mmasai mmoja aliyenukuliwa akisema kwamba "serikali inatakiwa iagize SPEED GOVERMENT za kuwazuia vijana waache ngono wajiepushe na UKIMWI, kuliko hizo vitu zinaekwaekwa kwenye MATATU." Wabunge kazi yao ni kutunga sheria, siyo kuwaelimisha wananchi sheria hizo. Kosa liko hapo.Wananchi wengi wanaogopa kupoteza muda mahakamani kwa mashauri yasiyoisha. Wananyimwa haki kwa sababu muda wa kuitafuta haki ni mrefu na hawana hakika kama wataipata haki yenyewe. Kwa maoni yangu serikali inapowapa polisi uhuru wa kuitumia sheria kuwanyanyasa wananchi, huo ni wizi wa mchana. Tofauti yake na wizi wa mabavu ni kwamba serikali inatumia sheria ambazo wananchi hawazijui ili kuwaibia. Na kwa kiwango hiki, serikali ndiye mwizi nambari wani.Majaji wanatakiwa kupima uzito wa shauri hata kama mshitakiwa amekubali kosa. Mazingira yanayomfanya akubali kosa yaangaliwe na ikiwezekana ushahidi kidogo utolewe na polisi husika ili washukiwa waachiliwe huru hata baada ya kukubali makosa. Mambo yakiwa hivyo tunaweza kusema Haki inaonekana kutendeka japo kidogo.Sheria zikiwepo ili kuwanyima wanyonge haki, basi wanajaribu kuzitii sheria wanakosea kufanya hivyo. Huwezi kutii kitu ambacho kuna watu wanaoweza kusema umekivunja na wakunyime haki ukiona na usiwe na pa kuwapeleka wala cha kuwafanya.Inauma kuliko ukoloni. Tena ni mbaya kuliko ubaguzi wa rangi.Ubaya wake unazidi pale wanaofanyiwa unyama huo ni wananchi wanaodanganywa kwamba wanaishi katika Kenya huru. Uhuru huo uko wapi wakati haki haitendeki? Waliposema ni mbinu ya serikli kuwahangaisha watu wa Matatu, ili wakubwa wawekeze kwenye sekta hiyo, sioni kama walikosea sana. Tayari wengi waliokuwa wakifanya biashara hiyo wameachia ngazi. Na makampuni kama CITY HOPPA yameshika usukani katika sekta ya usafiri Kenya. Hatuwajui wamiliki wake, lakini wanasema ni kampuni ya vigogo wa serikali. Na lisemwalo halipo labda liwe lilikuwepo hata kabla ya kusemwa.

Kibaki ajenga Hospitali ya kisasa Nairobi
Dr. Dan Gikonyo na mkewe Betty, mbele ya hospitali ya kisasa iliyojengwa katika mtaa wa Karen Nairobi. Dr. Gikonyo ni daktari binafsi wa Rais wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki. Hospitali hiyo yenye mitambo ya kisasa, inasadikiwa kuwa ya kipekee Afrika. Inaweza kufanya mambo mengi ambayo viongozi wa Afrika hulazimika kwenda ngambo kutibiwa. Kwamba Kibaki alifikiria kujenga hospitali kama hiyo Kenya, ni hatua inayostahili kupongezwa. Lakini gharama za matibabu katika hospitali hiyo ni za juu kiasi kwamba matajiri tu ndio watakaoweza kumudu. Itambidi Kibaki afikirie jinsi ya kuiboresha hospitali ya Kenyatta ambayo ndiyo hospitali ya rufaa nchini Kenya ili wananchi wa kawaida waweze kumudu gharama za matibabu. Vinginevyo itaonekana kwamba matajiri pekee ndio wanaostahili kuishi Kenya, na wengine wapotelee mbali.
Mitambo ya kisasa ndani ya hospitali mpya ya Kibaki. Kupimwa shinikizo la damu kisha ulazwe hapo wiki moja, ujue shamba na gari pamoja na akiba yako yote imekwisha. Omba Mungu azidi kukulinda na akupe afya njema kwani huwezi kumudu gharama za hapa. Ila pia jifariji kwamba hata hao wenye uwezo wa kutibiwa hapo, hufika mahali mitambo hiyo ikashindwa kuwasaidia na ikifikia hapo inawabidi wakubali kwamba Mungu pekee ndiye anayeweza kulinda afya zetu. Siyo vibaya wenye pesa wakijaribu bahati ya kujiweka hai wazifurahie pesa zao ulimwenguni. Lakini kwa muda gani?

Tangaza na GTV

 
| http://munishi.com |