Vs


NTV
Wavuta viatu badala ya Soksi
By Pastor Munishi





Je Kenya wata "Swich Off" NTV
au Itawa "Turn On"?
Kuboresha NTV
Haimaanishi kupora watangazaji kutoka KTN. Badala yake inaonyesha uvivu
wa kutengeneza watangazaji wenu, au kuwatafuta wapya.
Baada ya kurupushani na Lucy,
sasa Nation wanaonekana kushika adabu. TV yao wanasema itatuwasha badala
ya sisi kuiwasha.Wengi wametafsiri hiyo kama ongezeko la vipindi vinavyohusiana
na "ngono" Tayari wameanza kuonyesha nyimbo ambazo waimbaji
na wachezaji wako nusu uchi kama siyo uchi kabisa. Ikiwa walimaanisha
kuiwasha jamii kwa jinsi hiyo, basi wamekosea. Tunatakiwa kulaani vipindi
vya ngono kwenye TV. Na Nation wajue hivyo.
Kila la Kheri NTV
Tunapokaribisha mabadiliko
NTV, matarajio ya wengi yalikuwa kuona ubora wa vipindi NTV wanavyoweza
kutayarisha, na siyo kuvua watangazaji kutoka stesheni nyingine wakitumia
ndoano ya pesa. Ubunifu na kuandaa vipindi vingi kwangu huo ndio ubora
wa stesheni. Pesa siyo kila kitu. Ni kweli NATION wana kila kifaa ambacho
pesa zinaweza kununua. Lakini vifaa bila watu wabunifu ni bure. Wasishangae
mtu mbunifu mwenye KAMERA moja akafanya vitu vikawastaajabisha. Haijalishi
kipindi kimeandaliwa na watu wangapi, au na vyombo vya bei gani, kama
kipindi ni kibaya ni kibaya. Kuandaliwa NTV kwenye vyombo vya bei mbaya
hakukifanyi kipindi kuwa bora kama hakuna ubunifu wa kutosha
.
"LOGO"ya NTV
Inatia kichefuchefu
Baada ya kuwaza na kuwazua,
Nation waliona waje "LOGO" Mpya.
Nation TV walichofanya ni kubadili
"LOGO" lakini mtindo na mbinu bado ni ule ule. Tena wengi
wanasema sasa ndio wameharibu zaidi. Kama ulikuwa umezoea kupika maharage
kwenye chungu cha kawaida yakaiva na kuliwa, Ukinunua sufuria ya bei
ya juu na bado upike maharage, walaji hatutaona tofauti. Ndivyo NTV
walivyofanya. Kwanza aliyebuni hiyo "LOGO" hakutumia usanii
hata kidogo.Alichofanya ni kuiangalia "LOGO" ya CNN na kujaribu
kuiiga. Matokeo, alitengeneza kitu ambacho macho yetu yalishakiona CNN.
Ndiyo maana macho yanakataa kuamini kwamba NTV wana "LOGO"Mpya.
Fanyeni kiungwana. Rudini tena mezani, mchore upya. Huwezi kuja na kitu
kipya ambacho kimeshindwa ubora na kile cha zamani.
Wafanyikazi NTV
wamekosa motisha.
Mtindo wa NTV kuwanunua wafanyikazi
kutoka stesheni nyingine hasa KTN, unawafanya wale walioanza NTV kujiona
hawafai kitu. Akija Emmanuel Juma kutoka alikotoka, anapandishwa cheo
huku wakongwe wa NTV wanabaki midomo wazi kwa mshangao. Akija Nimro
Taabu kutoka taabuni, naye mara moja anawekwa kusoma habari huku kina
Shabani Ndege wakinyimwa nafasi ya kujiendeleza.

Kosa kubwa walilolifanya ni kumpa huyu Mwarabu toka KTN nafasi ya
kusoma habari badala ya Mukami ambaye anatawala "SCREEN" vilivyo.
Mukami sijui nimwite dada Mukami au Bi Mukami. Lakini tayari alikuwa
ameshapanda chati na kuwa kati ya watangazaji wazuri Kenya. Mwenyewe
akisoma Habari utadhani Natio TV ni mali yake.
Hesabu NTV
zinawachanganya pale walipomtoa Jamilla Mbogua na badala yake wakamweka
Bi Mohammed. Sina tatizo la udini, na pia sikubaliani na Jamilla pale
alipokuwa ameanza kuzidisha mapambo. Lakini ilikuwa ni kiasi cha kuambiwa
apunguze kujiremba kupita kiasi. Lakini kwa usanii wa kusoma habari
pamoja na kuweka madoido, hakuna mwenzake. Akikalia kiti na aangalie
camera, halafu aanze kuzungumza, Utadhani Nation TV ni ya Mbugua baba
yake. Hata kama angetoka nyumbani bila kunawa uso na asome habari bado
watu watamsikia. Jamilla ujue hivyo. Naye Sophy Ikenye anakosa nafasi
uwanjani kwani wachezaji wa kulipwa ndio wanaopangwa uwanjani hata kama
chenga zinawashinda. Wafanyikazi wengi wanasema hiyo siyo sawa. Huwezi
kuja utukute, halafu uwe Boss wetu. Sisi ndio tunaotakiwa tukuonyesha
mambo hapa hufanywa vipi. Ila NTV wanafanya kinyume chake.
NTV ni Walafi
Kifupi niseme NTV
wamevimbiwa. Ulafi wa watangazaji umewafanya wale kupita kiasi na sasa
WAMEVIMBIWA. Matokeo wengi watakuwa "WASTE". Sio ajabu, kwani
sera za Nation ni kununua kila mtangazaji KTN wakifikiri kufanya hivyo
kutaiporomosha KTN. Walidanganyika. Sasa wameonyesha kila mtu kwamba
KTN ilikuwa inawakosesha usingizi. Wengi wanasema kama mmewachukua,
basi wafanyeni bora kuliko walivyokuwa. Kinyume cha hayo NTV itaonekana
kana kwamba nia yao ni kuharibu vipawa vya watangazaji wanaonunuliwa.
Unaulizwa wewe ni bei gani, ukisema, unanunuliwa ili uharibiwe uwe "WESTE"
Hata watangazaji wanaohama kila kukicha, na wenyewe wana kasoro ya Tamaa.
Wanataka huku na huku, mwisho watakosa kote.
Maringo NTV
Hayatawasaidia





Bennie Mack Ambaye TV nyingi Afrika hununua maonyesho yake kwa mamilioni
ya dola.
Nani alisema kwamba vipindi
vizuri lazima vitoke Marekani? Kwamba Nairobi wameanza kutengeneza mikanda
ya video hizo ni habari njema. Inashangaza kuona kwamba TV Stesheni
nyingi hazijapokea habari hizo kwa furaha inayozistahili. Hakuna hata
stesheni moja iliyoanza kununua video hizo na kuanza kuzionyesha. Kwao,
kwenda Marekani kununua maigizo ambayo hayaendi sambamba na tamaduni
zetu ni rahisi, kuliko kuteremka River Road na kununua maigizo ambayo
wengi tunaweza kujihusisha nayo. Wanadai ubora wa picha ni duni. Kila
kitu lazima kianzie mahali.Ikiwa wale wanaojiita waandishi wa habari
hawajaweza kuzalisha igizo lolote, siyo ajabu soko la video za nyimbo
za Injili likaanzia River Road. Majumba ya TV yameze kiburi na wafanye
kile ambacho kila mtu alikusudia wafanye. Debe tunalolisikia Nation
lilenge kununua kazi za wasanii humu nchini na kuzionyesha. NTV waache
maringo na waanze kuonyesha maigizo na nyimbo zinazotengenezwa na wasanii
humu nchini. Kiwango cha ubora kisiwasumbue bali waangalie sanaa iliyotumika.
Hata HOLLYHOOD haikuanza na ubora walio nao. Lini waafrika watajifunza
kujivunia chao? Leo hii ukipeleka nyimbo yako NTV na wajue ilitengenezewa
River Road wanaidharau na kuitupa kapuni. Lazima muwape moyo wasanii
wa humu nchini ili kazi zao ziweze kufikia ubora wa kina OPRAH. Haiingii
akilini kuona stesheni inatumia mabilioni ya shilingi kuagiza vipindi
kutoka nje wakati wasanii wa humu nchini wanawapelekea kazi zao wazionyeshe
bure bila malipo lakini wanawapuuza. Badala yake waliopaswa kulipwa
ndio wanaolipa ili kazi zao zionyeshwe kwenye NTV.
Ikiwa mabadiliko yalimaanisha ongezeko la vipindi vya ngono kutoka Marekani
basi NTV wamepotea lengo.
Hiyo ni AIBU
kubwa. Ni matumaini yetu kwamba mabadiliko NTV yatalenga kuinua wasanii
wetu. Kinyume chake ni kuendeleza utumwa wa kimawazo ambao vyombo vya
habari Afrika vimekuwa vikiukumbatia kwa muda mrefu. Mtasemaje kuhusu
vyombo vya habari Afrika kujaza kazi za wasanii wa nchi za magharibi?
Huo ni Utumwa wa kimawazo. NTV Onyesheni mnamaanisha mnaposema mna mipango
ya kuboresha stesheni yenu.
NTV wavuta Viatu badala ya Soksi
Anaitwa Sophy Ikenye
Je Kenya wata "Swich Off" NTV
au Itawa "Turn On"?
Kama kuna jambo linalowakera
wakuu wa NTV, ni pale wanapomweka mtu kusoma habari na mtu huyo anajulikana
kuliko wao. Nasikia hilo ndilo linalowafanya wabadilishwe kila kukicha.
Wengi tunaliona hilo kama usumbufu. Kama wanataka, na wao waingie uwanjani.
Tunasubiri NTV Jioni itakayoletwa na Bwana Kiboro.
Nation Kenya
ni Kiboro japo mmiliki ni Agha Khan

Bwana Wilfred Kiboro akiwa na Agha Khan Mmiliki wa Nation Media.
Nation ilianzishwa mwaka 1960 na Shehe wa dini ya Kiislam Bwana
Agha Khan. Kinyume na KTN iliyoanzishwa mwaka 1989 na wafanyibiashara
Wakenya. Kinachowashangaza wengi ni Nation kununua watangazaji kutoka
KTN badala ya kinyume chake. Hatujali nani ananunua nani, Lakini kufanya
hiivyo kuzuia upinzani ni kosa. Haki ya Nation kuboresha NTV siyo lazima
izime zile TV nyingine. Ubora wa NTV utapimwa na KTN yenye nguvu. Kutumia
pesa kuwamaliza wapinzani kama GTV hakutaifanya NTV bora. Badala yake
NTV itakuwa dikteta wa habari. Uhuru wa vyombo vya habari utatoka wapi
wakati vyenyewe vinanyimana uhuru? NTV inapodai uhuru wao kuhabarisha,
huku ikiwanunua wanahabari kutoka KTN na zile stesheni nyingine (Lakini
siyo GTV), Huo ni unafiki unaotakiwa kukemewa kwa nguvu zote. NTV
wanatakiwa wajue kwamba pesa siyo kila kitu. Kiboro anaweza kucheka
mpaka jino la mwisho leo, Lakini kama siyo AGHA KHAN Nguzo kuu ya Nation
Mwenyewe angeanzisha "KIBORO TIMES" ingefika wapi?
Bwana
Joseph Muliro Akijibu hoja kwa niaba ya NTV, Alisema:
" Hellow sir Well thanks for your comment but I would beg to
disagree with you, both Nation TV and radio started in 1998, while KTN
atrted in 1991, The Nation News paper started in 1968, while standard
news paper started in 1902. secondly NTV is the only station that shows
african movies like wingu la moto, another one is UHONDO, while KTN
doent have even a single African movies, thirdly when it comes to christin
music, Nation TV is the leading station when it comes at playing gospel
songs and we have a programme called the storm every saterday.coming
to the issue of presenters, Nation has never approached any KTN presenter
in the name of giving him/her more money, we normally run those job
vacancies in the news paper, and any body is free to apply, on the contrary
KTN took most of our presenters, watch Nation and watch KTN and you
will come to right conclution, good day sir."
Ni
maoni yake kama alivyoandika mwenyewe. Gazeti la Injili hatukuhariri
chochote.
Je! Una maoni Gani? Tuandikie kwenye fomu mwisho wa ukurasa huu.
MAURICE MUNENE MUGAMBI. mrcmunene@hotmail.com Asema:
UKWELI MTUPU KUHUSU NTV.
Naunga mkono maoni yako, kuhusu
hulka mbaya ya mabwanyenye wa Nation,kuwawinda wasomaji habari kutaka
KTN.Hatuijaona 'any added value'baada ya wao kuwachukua. I also ask,who
says Munish cant rule Tanzania?These prophets of doom will be proven
wrong soon for God is surely lifting you from one level of glory to
another.God gives mandate. Unlike many Kenyan polictian rebels,without
a cause,you surely stand out as visionary leader for your country. However;i
believe your true patriosm can be demonstrated better if you opted to
fight from within and not without.Am afraid History may judge you rather
hashly because you aren't alone in this battle-Your brothers from within,Tanzania,are
taking the bull by the its horns through an organised political vehicle.Though
they are various of them ,i strongly believe you should board one and
further the common cause in an unified voice.What's your take on this
ndugu Munishi? Otherwise you are a true son of Africa.You should fire
from all angles and don't spare your host Kenya too.We need to hear
your thoughts about the powers that be in Kenya.You are hero at home
and heros are saluted everywhere not because they are always right but
because they are always principled. I would love to hear from you.

Huyu ni Bwana Lui Otieno KTN. Anasema yeyote
anayetaka kuujua ubaya wa NTV awasiliane naye kwa simu. Alikuwa huko
yakamfika shingoni akatoka. Anawajua NMG ndani na nje. Kwa sababu NTV
wamesema, yeye atasema akiulizwa kufanya hivyo. Nanyi waomaji wa GTV
On line, Msiandikie mate wakati wino uko. Nambari ya simu hiyo hapo.
Kwa wale walio nje ya Kenya itawabidi watangulize nambari ya kimataifa
+254 kisha ufuatishe nambari zinazofuata. Wasomaji, Lui Otieno huyu
hapa. Muulizeni yanayowakera moyoni. Wengine wamekuwa wakiuliza kama
ameoa au la. GTV hatuna majibu, Lakini Lui mwenyewe atawajibu.

KBC wasema wao ni "JUNGU KUU HALIKOSI UKOKO"

KBC walipowaona NTV wanavuta viatu na havivutiki,
wao waliamua kuvuta soksi zao. Walikuja na mbinu mpya ya "Jungu
kuu halikosi ukoko." Walienda kwenye Maktaba yao na kuchukua maigizo
na filamu za zamani na kuziita zilizopendwa. Sasa watazamaji wanaonyeshwa
zilizopendwa. Hiyo tu imewapa NTV kibarua kigumu. Sasa watazamaji waliokuwa
wawekwe sawa na NTV, wanazunguka kila mahali mradi wapate kipindi kizuri.
Mawazo ya NTV kwamba watazamaji wangeikodolea macho NTV pekee, yamegonga
mawe. Labda warudi tena mezani kuchora upya. Kijisanduku kwa jina TV
kimepata sura mpya baada ya utitiri wa vituo vinavyoitwa vya TV kuanza
kurusha matangazo bandia. Sasa mtazamaji ana uhuru wa wa kutotizama
zote, na kujitengenezea utaratibu wake wa nini aone na kwa wakati gani.
Shukrani kwa vifaa vya kuchezea VCD. Wengi siku hizi wanajinunulia VCD
zenye nyimbo za Injili kutoka wasanii tofauti na kuanza kujipangia utaratibu
wa vipindi vya kuona kinyume na ilivyokuwa mwanzo, Eti wangoje kuwekewa
vipindi na NTV wakati wao wenyewe ni TV stesheni. Wamegundua kwamba
NTV na zile nyingine wanachofanya ni kuweka mikanda ya nyimbo na filamu
kwenye chombo kama VCD Player au Video Player. Tofauti ni kwamba mitambo
ya kurushia matangazo hupeperusha hewani kilichowekwa na kukiingiza
kwenye nyumba za watu kupitia erial zilizotundikwa juu ya mapaa ya nyumba.
Wengi wanasema indapo TV hazitabadili mtindo, basi itawalazimu kuondoa
vifaa hivyo juu ya nyumba na kutegemea vipindi wanavyojipangia wenyewe
nyumbani mwao.
CITIZEN nao sasa wameamka.
Wameboresha mitambo ya kurushia matangazo.
CITIZEN nao sasa wameamka. Wameboresha
mitambo ya kurushia matangazo. Wanapatikana kiurahisi hata kama eria
imeelekezwa popote. Wamegundua kwamba walio wengi hawasumbuki kurekebisha
erio zao. Ile TV inayopatikana ndiyo inayoangaliwa. Ukiangalia
juu ya mapaa ya nyumba za watu Afrika, utagundua kwamba chombo kinachopaswa
kunasa matangazo ya TV kimewekwa kiholela sana kiasi kwamba kama huna
mitambo ya nguvu na iwe kila mahali ni vigumu TV yako kuonekana. Watu
wengi hawako tayari kuwalipa wanataaluma wawawekee erio kiutaalamu.
Ndio maana utaziona zimeelekezwa popote na mara nyingi huwa hazilengi
mitambo yeyote. Siyo ajabu kukuta mtu yuko karibu sana na mitambo ya
kurushia matangazo ya TV na bado TV yake inaona mchele badala ya picha.
CITICEN wamegundua hilo, lakini bado wanahitaji kuvuta soksi zaidi.
Wanadai wanasikika na kuonekana Arusha na Uganda. Lakini GTV ilipowasiliana
na Arusha walisema hawajaiona CITIZEN huko. Ila katika kuifanya TV yao
kuonekana ya Afrika tena Kenya, CITIZEN wanaongoza kwa hilo.
Je TV
zinazojiita za Injili ni bora kuliko zile nyingine?
Nazo TV zinazojiita za
Injili hazitofautiani sana na zile za kidunia. Gharama za kutangaza
mikutano ya Injili ni juu kuliko kawaida. Zimejibandika majina kama
Family Media lakini ni TBN. Ukidanganyika ufikiri ni TV ya humu nchini
inayojali maslahi ya wahubiri wa humu nchini, Hutayaamini masikio yako
pale utakapoambiwa ulipe kwa DOLARI za Kimarekani ndipo uweze kuonekana
hapo. Cha ajabu bado wanachangisha pesa kuwawezesha kurusha matangazo
yao nchi nzima. Kwao Waafrika ni watu wa kuhubiriwa tu na wahubiri kutoka
Marekani. Kwamba TBN wanadhamini Family Media na vipindi vyao ndivyo
vinavyopewa kipau mbele, huo ni ukweli usiopingika. Lakini kutulipisha
pesa wahubiri Waafrika ndipo tuweze kuonekana hapo, na kisha kutuchangisha
ili kuisaidia TV iliyokwisha changiwa kutoka Marekani, ni sawa na kutuibia
mchana. Wahubiri imewabidi wawe matapeli kuweza kupata pesa za kulipia
TV zinazojiita za Injili. Wengine imewabidi kutengeneza miujiza ya uongo
ili watazamaji washawishike kuwapa pesa ambazo nao huzipeleka mifukoni
mwa Family Media TBN. Tunapowalaumu wahubiri matapeli, tutakosea sana
kutozilaumu TV zinazowafikisha katika hatua hiyo. Ziwe ni zile za kidunia,
au zinazojiita za Injili, haziwezi kwepa lawama. Ni haki ya watazamaji
kuhabarishwa na kuelimishwa, lakini vyombo vya habari vinapodhamini
pesa kuliko watazamaji na wasikizaji wake, Hatari iko hapo. Pesa mbele
Injili nyuma, ndilo changamoto yao. Wakristo walifarijika wakati TV
nyingine ya kidini ilipoanza kurusha matangazo yake Nairobi. GODS TV
chini ya kivuli cha SAYARE TV kutoka kule Eldoret, imeanza kufanya kile
watazamaji walichokizoea kutoka Family. Yaani mahubiri kutoka kwa wahubiri
wa Marekani. Wanadai kwamba minara ya kurushia matangazo imegharimiwa
na GODS TV, na masharti ni lazima masaa kumi yawe ni yao GODS TV. Ni
Masharti kama hayo ndiyo yanayotufikisha kusema kwamba inaonekana Waafrika
hawajafikia wakati wa kuanzisha TV zao za Injili. Kama wamefikia basi
waanzishe TV zile ambazo haziwekewi masharti yeyote na TV za Kimarekani.
Tunausubiri wakati huo kwa hamu. Lakini kwa sasa lazima tuvumilie Family
TV ikiwajenga kina TD JAKES na wengine kutoka Marekani, Ili siku watakapozuru
Kenya wapokelewe kuliko Rais. Wakiondoka watuache tukigombania Dala
kidogo walizotuachia. Tena sasa lazima tuikaribishe TV nyingine kutoka
huko huko Marekani kwa jina la SAYARE. Nao watafanya kile kile Family
na CITICEN wanachofanya. Kuwapatia masaa wakubwa waseme kwani wamesaidia
kuweka mitambo ya kurushia matangazo. CITIZEN ukiwasikia wakitamba kwamba
wao ni pale roho ya nchi inapodundia, Wanakingiwa kifua na VoA ya Marekani.
Ukoloni huu wa kutawaliwa kwa kutumia vyombo vya habari utaisha lini?
Nani atukomboe? Mungu atusaidie.





Kiboro ametoka Nation yakarabatiwa

Gazeti la Nation kwa mara nyingine
wamegeuza sura, Baada ya mkurugenzi wa zamani bwana Wilfred Kiboro
kuonyeshwa mlango. Mkurugenzi mpya amekuja na mbinu mpya. Ana kibarua
kizito kurudisha heshima ya Nation kama gazeti linalozingatia maadili
ya taaluma ya uandishi habari.
Miaka sita iliyopita waligeuza sura bila
mafanikio, na sasa wanaonekana hivi. Wanadai wataalamu wao walikaa
takriban miezi tisa kubuni mpangilio wa Nation inavyoonekana sasa.
Pamoja na majigambo hayo, pia NTV ilitangaza LIVE wafanyikazi wa shirika
hilo wakiuza magazeti yenye sura mpya kwenye barabara za Nairobi.
Kilichowashangaza wengi, ni jinsi walivyoitumia TV kuwalazimisha watu
watoe maoni waliyotaka kusikia. Asubuhi saa kumi na mbili na nusu,
NTV walionekana wakichukua maoni kutoka kwa watu waliowaita wasomaji,
na wote walionekana wakiwamwagia sifa tele kuhusu muundo wao mpya
wa gazeti pamoja na mpangilio wa makala. Wengi tulijiuliza wamesoma
saa ngapi na kufikia hatua ya kusifu au kukashifu? Japo hakuwepo wa
kuwakashifu. Nimroho Taabu alikuwa studio, wakati Shaaban Ndege alikuwa
barabarani akiwahoji kuanzia wauzaji na wasomaji, na hata wafanyikazi
wenzao ambao siku hiyo waligeuka WAMACHINGA wa kuuza magazeti. TABU
alipomuuliza Shabani vipi kuhusu kurasa za gazeti hilo ambazo awali
zilikuwa 30 na sasa ni 72, Jibu lilikuwa watu wamezifurahia sana na
ndiyo maana wamesoma haraka na kumaliza na saa moja kamili wanatoa
maoni yao jinsi sura mpya ya Nation ilivyowavutia. Iliwabidi NTV wafanye
kile ambacho hawafanyi yaani kuwa na kipindi cha leo magazetini. Tofauti
na KBC pamoja na CITIZEN, Leo magazetini ya Nation ilikuwa na gazeti
moja tu, nalo ni Nation Mpya iliyokuwa inajiuza na siyo kujitembeza.
Lakini wengi waliiona hatua ya NTV kujipigia
debe asubuhi kama kibaya kinachojitembeza. Japo mimi siku hizi sinunui
magazeti, lakini siku hiyo ilinibidi ninunue nione jipya ndani ya
Nation mpya. Sinunui magazeti kwani kila asubuhi KBC hunisomea magazeti
yote kwenye kipindi chao cha DAMKA na KBC channel one.Lakini tofauti
na siku nyingine, siku hiyo walionyesha kichwa cha habari katika Nation,
lakini siyo nembo yao. Kwamba wanatumia magazeti yao kila asubuhi
kuwafanya watazamaji watizame kipindi chao cha leo magazetini, na
leo gazeti mojawapo limegeuza sura yake na KBC wakatae kuonyesha,
hilo kidogo lilinikera. Ikiwa vyombo vya habari vinaogopana kiasi
hicho, kwa nini KBC wayatumie magazeti kutayarisha kipindi huku wakiwanyima
wenzao haki ya kuonekana kwenye TV yao wakati wanapogeuza sura ya
gazeti lao? Hayo tuwaachie wenyewe, wanajuana kwa vilemba. Nilipolinunua
gazeti la siku hiyo kweli kulikuwa na mabadiliko. Pengine siyo kama
wenyewe walivyotia chumvi nyingi, lakini binafsi niliona kuna mtizamo
mpya wa masuala hasa ya siasa na kidini.
Japo walijigamba kwamba iliwachukua miezi
tisa kuunda mpangilio wa herufi na sehemu za kuweka picha pamoja na
LAYOUT nzima ya gazeti, mimi niliona kwamba kazi hiyo ukimpa mpiga
chapa anayejua kutumia PAGE MAKER, itamchukua muda usiozidi masaa
mawili kuja na mpangilio mzuri kuliko huo wa Nation inayoitwa mpya.
Lakini kwenye maoni ya mhariri walionyesha
kwa mara ya kwanza kuipinga Serikali ya Kibaki kwa kile walichokiita
mwingilio wa serikali kuusambaratisha upinzani kama CCM inavyofanya
huko Tanzania. Pia walifanya kile ambacho wengi hawakukitarajia kwani
kwa miaka ya hivi karibuni Nation ilionekana kulegeza kamba na kuinamia
upande wa serikali. Kwenye toleo lao jipya walimwambia Kibaki usoni
kwamba kama mbinu anazotumia zinalenga kumrudisha madarakani kwa gharama
yeyote, basi mambo yatamwendea kinyume. Walienda hatua zaidi na kuchora
katuni ya Kibaki akiletewa barua isemayo ODM wamemngatua madarakani.
Kwangu hiyo ni hatua nzuri kuelekea pazuri. Serikali hazipaswi kuumaliza
upinzani ndipo zijigambe kwamba zimerekebisha uchumi.Serikali nzuri
ni ile inayoruhusu upinzani wenye nguvu, na wakabiliane nao bila kutumia
hila, wala nguvu ya dola kuunyamazisha upinzani.

Kwa nini Rais wa Tanzania hasikiki duniani
kwa lolote? Kila mtu anajua kwamba serikali ya nchi hiyo hutumia vyombo
vya dola kuwanyamazisha wapinzani. Hata kama wangeenda mwezini kwa
miguu, bado dunia itawadharau serikali ya Tanzania kwani wanajua mbinu
wanazotumia kubaki madarakani. Katika hilo la kumuonya Kibaki asiufuate
mkondo wa watu kama kina Kikwete tunawapongeza Nation. Pia walimchokonoa
Paul Kagame wa Rwanda na kumuusisha moja kwa moja na mauaji ya halaiki
ya Rwanda.Pamoja naye pia walimlaumu Yoweri Museveni wa Uganda kwamba
alihusika kwa njia moja ua nyingine katika kumsaidia Kagame aiangushe
ndege iliyokuwa imembeba rais wa Rwanda wakati huo, na kusababisha
mauaji ya halaiki. Katika hilo pia Nation mpya wana pongezi zetu.
Isitoshe katika toleo hilo, walimsakama baba mtakatifu na kanisa Katoliki
kwa kuwanyima uhuru makasisi waliolemewa na tamaa ya wanawake waoe
na waendelee kuwa makasisi wa kanisa hilo. Walimnukuu askofu Emmanuel
Milingo akisema kwamba atawatawaza makasisi waliooa wawe wahudumu
katika kanisa hilo la kikatoliki ambalo makasisi wake hujifanya hawaoi,
huku wakiongoza katika ufuksa, hususan wa kufanya mapenzi kwa watu
wa jinsia moja. Kama hayo ndiyo mabadiliko waliyomaanisha Nation,
basi tunawapa mkono wa kheri na kuwaombea wasibadili msimamo huo.
Lakini wana kazi kubwa kutuhakikishia kwamba wamejikomboa kutoka mikono
michafu ya serikali iliyotaka kuwageuza kama wapiga debe wa serikali.


Nation ilianzishwa mwaka 1954 na tajiri
wa kihindi Bwana AGHA KAN. Magazeti hayachaguliwi kama wabunga na
Rais, kwa hiyo ni vigumu kujua lini Nation watangatuka madarakani
wayaachie magazeti mapya yaje na mitizamo mipya. Kanu iliikuta Nation
na imetolewa, na bado hawa jamaa wanaendelea kujibadilisha ngozi kama
nyoka. Kama ilivyo kwa wanasiasa, Gazeti likilewa madaraka hufikia
hatua ya kuamua nani awe nini na kwa muda gani.Tunaomba Mungu Nation
isiwe inaelekea hapo. Lakini wenyewe wanajiona hapo. Ndio maana utawasikia
wakisema wanatafuta wasanii wapya, wanasiasa wapya, lakini siyo magazeti
mapya. Wakati sasa umefika wa sheria kuundwa ili kipindi cha magazeti
kisizidi miaka 10 na tena yale yanayochapisha yawe yamechaguliwa na
wananchi. Yaani uchuguzi mkuu pia uvihusishe vyombo vya habari. Unafikiri
kama siyo kura, lini kina BBC na CNN, na sasa NATION watatoka madarakani?
Vyombo kama GTV haturuhusiwi kukua nasi tutoe maoni tofauti na hawa
wanaojiona wanahabari wa maisha. Nation wana TV yao ambayo wimbo ambao
hawakuurekodi wao lakini una alama ya GTV hawauonyeshi. Kisa hawatambui
chombo kingine cha habari.Tunapoimba kuhusu demokrasia, lazima tuelekeze
macho yetu kwa vyombo vya habari ambavyo vimetawala kwa muda mrefu
wa kutosha. Vitoke viwaachie nafasi wanamapinduzi wenye mawazo mapya.
Magazeti kama UHURU na MZALENDO ya Tanzania, hayapaswi kuwepo kwenye
ulimwengu wa sasa. Lakini kwa sababu yanamilikiwa na Serikali mbovu
ya CCM, basi yanaendelea kuudanganya umma wa Tanzania kwa propaganda
zinazoitwa habari. Serikali yenye siasa mbaya ya ujamaa na kujitegemea
inapomiliki vyombo vya habari Tanzania, utatarajia siku moja kusikia
kutoka vyombo hivyo kwamba siasa hiyo ya kujitegemea kiumasikini ilishindwa?
Ndio maana kuna haja ya kuvipigia kura
vyombo vya habari. Na hapo ni kama havitatumia mbinu chafu wanazotumia
CCM kubaki madarakani hata leo. Lakini nafasi itakuwa imetolewa kwa
vyombo vipya vya habari kuingia uwanjani. Kama kuna uwanja mgumu kuingia
na kucheza duniani, ni uwanja wa vyombo vya habari. Lakini tunashukuru
teknolojia kwani hata haya ninayoyaandika usingeweza kuyasoma kama
siyo mtandao wa Internet. na huku pia kuna majabali kama kina GOOGLE
na YAHOO ambao nao wanajiita wababe wa mtandao.Uzuri wao hawa wa hapa
wanaruhusu wengine waonekane hata kwenye sachi injini zao. Nina maana
ukichapisha www.gospelgtv.com na uwaambie GOOGLE au Yahoo wakutafutie
iko wapi, watakuletea bila wivu.Nation hawawezi fanya hivyo. Wanajifikiria
wenyewe kwanza kabla ya wengine. Wanataka kila mtu angatuke au kustaafu,
lakini siyo wao.
Nation
Lageuka kuwa Gazeti la chama na serikali 
Hatutegemei kazi ya gazeti iwe ni kuipinga serikali tu, Sambamba na
hilo hatutegemei gazeti liwe linaimba sifa za serikali hata pale serikali
inapokosea. Nation wanafanya hivyo bila haya. Tangu serikali mpya
waingie madarakani gazeti la Nation limekuwa likiyafumbia macho makosa
yao, huku wenzao Standard wakiwa mstari wa mbele kuyakemea. Baada
ya Nation kuisoma "Stori" hii, Kiranja wao Wilfred Kiboro
alikasirishwa sana. Haraka aliamuru sera za gazeti hilo zibadilishwe
na kuanza kuikemea serikali. Sasa kama hawaikemei serikali kwa sera
mbovu za usafiri, Kiboro mwenyewe anakuwa habari, kama siyo habari
kuwa Kiboro. Walianza na Kibaki mwenyewe pale waliporipoti kwamba
aliporomoka kwenye ngazi za Ikulu na kutonesha majeraha ambayo tayari
alikuwa nayo. Serikali iliwapuuza kwani ilikuwa na kazi ya kuwanyamazisha
Standard waliokuwa wamezidi na kelele zao. Ni ukweli usiopingika kwamba
Nation ya Kiboro inaboronga na inaporomoka, huku Standard wakijigamba
kwamba wameshika usukani. Sijui kama wasomaji watarudisha imani yao
kwa Nation tena. Tunasubiri tuone. Serikali ni kama inafanikiwa. Kwani
Standard nao wanaonekana kwamba mdomo waliokuwa wakiupanua sana kupiga
kelele, umewekwa kitu, na sasa sauti haitoki sawasawa. Kwamba wanaopinga
ndio wanaozawadiwa, inaonekana kuwaumiza Nation na CITIZEN. Sasa wameanza
kupinga. Lakini wakiwa wamechelewa. Nani aliwadanganya wanasiasa watakumbuka
fadhila? Wanajidai kuwasaidia Kana kwamba wanajitetea, Nation waliandika
kuhusu mhariri wa gazeti hili na kujaribu kuichambua web site hii.
Lengo ni kuonyesha kwamba mkuki kwa Nguruwe ni sawa, lakini kwao ni
wa uchungu.
Habari zaidi





Rev.Wachira asema magazeti yanapaswa kuikosoa serikali, kwani
hata kama serikali ingeundwa na malaika, bado inahitaji chombo cha
kuikosoa isiende mrama. Ni makosa kufikiri kwamba serikali mpya haijafanya
makosa. Kwangu tayari wamefanya makosa mengi kwa mwaka mmoja madarakani.
Mwaka wa pili utakuwa kuvunja rekodi ya makosa yaliyofanywa na serikali
za awali.Tusubiri hadi wavunje rekodi ndipo tuikosoe?

Mfano gazeti la Nation, Limeacha sera zake za karibuni za kuisifu
serikali ya Kibaki, na sasa wameanza kumshambulia Munishi.
How politics derailed
the Munishi gospel crusade
By DAN TENG’O
He came, he saw and conquered the local gospel music scene. But not
any more. The lustre that Faustin Munishi had in the 80s when he took
the local gospel music scene by storm seems to have faded out.
The once-famous artiste, who popularised solo gospel music in the
early 1980s when the genre was dominated by choirs, is no longer enthralling
fans with hypnotic vocals and idiomatic Kiswahili rich in imagery
and symbolism as he used to.
Since 2000, when the Tanzanian Government banned the evangelist’s
seventh gospel cassette titled, Mpende Adui (Love the Enemy) owing
to its political views, nothing has been heard of him, at least musically
speaking.
Instead, the Arusha-born Munishi has remained steeped in political
activism for the past few years and has now decided to fight for his
cause via his website.
Munishi, who is credited for rocking the local gospel music scene
with seven delightful music albums, has vowed to censure Tanzania’s
ruling party, Chama cha Mapinduzi (CCM), until its downfall, of which
he seems sure.
On his website, which is full of his family pictures, Munishi claims
that he has been "anointed by God" to free Tanzanians from the country’s
ruling party. To hammer the point home, Munishi attacks the party
with acid lyrics of the opening track for the album Mpende Adui.
In true vitriolic fashion, Munishi’s website has a link entitled
"Wasikilize waongo!" (Listen to the liars! which, upon clicking, directs
one into the Tanzanian National Website.
He takes a swipe at President Benjamin Mkapa’s government, accusing
it not only of misruling Tanzania, but also of human rights abuses.
He cites himself as an example of a gagged citizen, saying copies
of Mpende Adui were confiscated by police for allegedly disparaging
the Mkapa government.
"Tanzania is for all its citizens and not Mkapa’s or CCM’s
as it seems to be," he trumpets in his website, adding that Mkapa
claims to know everything that is good for Tanzania yet the opposite
is true.
On the website, he hits at the US virulently, much as he did in the
song titled Msiabudu America (Don’t worship the US), featured
in his controversial seventh album. In the song, he accuses the US
of denying people visas unnecessarily.
Also on the receiving end of Munishi’s attacks are journalists
and local media houses with the exception of KBC (Kenya Broadcasting
Corporation), which helped to boost his musical career back in the
mid-eighties and BBC which granted him a full interview during his
tug-of-war with the Government of Tanzania, which he confesses to
hate.
He rails at radio stations for being overly commercial. "Their aim
is not to inform or entertain. They are out to broadcast commercials.
They use commercial means to target believers, thus injuring their
faiths. Their programmes gloss over matters to do with faith," he
says.
Before finding a vocation in music, Munishi, 44, worked as a painter
in Arusha. In 1980, he acquired an accordion and started to sing old
Sunday school themes such as Niko Chini ya Mwamba which became a number
one single in Kenya.
Munishi became a born-again Christian that year and joined Tanzania’s
Bishop Mosses Kulola’s entourage as a singer before ditching
the old preacher for a solo music career in Nairobi.
His debut album registered mild success. The second, Niko Chini ya
Mwamba, however, put the singer into big business. In 1989, he went
back to Arusha and married Ms Prisca, with whom they sang a duet in
the opening track for the third album "Yesu na Wewe" (Jesus and you).
From then, the wife never sang in public again, thus causing the wide
speculation that she had actually ditched the singer.
In 1993, Munishi made another trip to Arusha (in a sleek white Mercedes
Benz) to refute the allegations and did it at an open-air crusade,
where the alleged estranged wife accompanied him in a musical number,
just to prove that she was still around.
Munishi is blessed with three children, the oldest being Mojashi,
who immediately after being born, joined the father's singing group
in Nairobi by the name "Mojashi Choir".
The choir collapsed later and so did Munishi’s own newspaper,
Injili, whose first and only copy came out in 1996.
Most of the newspaper material has been repackaged in his website
which, like the print version, is full of Munishi’s various
profiles in the positive and his "enemies" in the negative.
Munishi Bado nahubiri Injili
Nashukuru
kwamba wengi wameanza kunielewa. Lakini kuna wale ambao bado kwa makusudi
hawataki kuelewa kwamba Munishi mimi sijaacha kuihubiri injili. Ila
wanakataa ukweli kwamba Injili ni maisha na sijui wapi utajenga ukuta
useme injili inaishia hapa na siasa inaanzia hapa. Katika hilo tukubaliane
kutokukubaliana.
Kwangu kuikemea CCM na serikali mbovu ya Mkapa, ndiyo Injili yenyewe
hiyo. Injili inakataa maovu ya kila aina. CCM aliyoanzisha Nyerere
ni baba wa maovu Tanzania. Ndiyo maana kwangu ni sawa na JEHANAMU
Tanzania.
Sasa magazeti yameanza kunishambulia eti nimejaribu kusema nitakuwa
Rais wa nne Tanzania. Kuna ajabu gani mimi kuwa Rais? Nina kila kinachohitajika
kuwa Rais wa Tanzania.
Vyombo vya habari vijue hivyo na viache kunisakama.