![]() ![]() |
||
BBC gospel TV gospelradio Gospel radio gospelnews Gospel
news |
Wana
furaha ya asili ambayo haipatikani kwenye pesa na mali za dunia hii.Wanatosheka
na kile walicho nacho.Kwao vitu siyo muhimu sana.Leo unaweza uwakute
na simu ya bei ghali sana, lakini wakisikia njaa hawatajali kuiuza
bei sawa na bure, mradi wapate furaha ya siku hiyo.Hawajali kama wana
gari au la, hujiona huru wakiwa bila. Kile ambacho hawakosi ni jinsia
ya kike karibu nao.Wakiwaona watoto kama wanavyowaita, husisimka utafikiri
ni roboti zilizopigwa funguo.Usijali kama watakayokuwa wakisema ni
kweli,hata wenye jinsia hiyo ni kama hupenda wadanganywe. Utawasikia
wakisema wao ni watoto wa matajiri wa Kenya. Eti baba yao ndiye mmiliki
wa vituo vyote vya petroli Nairobi.Hutumia hiyo kama ndoano ya kuwanasa
kinadada wanaotafuta kazi. Mbinu nyingine wanayoitumia ni ile ya kusema
wanaweza kuwasaidia wanaotaka kunakili nyimbo zao kwenye CD au kaseti
na hata video. Hujigamba kwamba wana studio za kisasa jijini Nairobi.Mungu
apishe mbali usikute hawa kinadada wa familia moja wamenasa kwenye
mtego wa Sammy.
Wengi hujiuliza kwa nini maisha ya vijana hawa ni kama maigizo? Huwezi kutofautisha wanapomaanisha na wakati wa maigizo. Mara nyingi wamekosa kuaminiwa, na hata kusingiziwa, kwa sababu ya usanii wao katika kila jambo. Mfano wanaweza wakuombe nauli ya basi kwenda mahali fulani, uwakatalie kwa sababu tu wanaigiza utajiri ambao kweli haupo.Wenyewe wanakiri kwamba wamewekwa kwenye ulinzi mkali na wake zao kwa sababu hawawaamini. Kila mmoja ameoa na wamejaliwa na watoto. Yale ambayo kila mtu alishindwa, wake zao wameyaweza. Tangu waamue kuishi na mke mmoja kwa zaidi ya miaka mitano, maisha yao yamebadilika kwa kiwango kinachowashangaza wengi.Hata wenyewe wanashangaa.Wanasema hawakuamini kwamba siku moja wangewekwa chini ya ulinzi mkali namna hiyo. Kama wanavyodai, hawakujua waliingiaje kwenye mtego na kujikuta wakiwajibika kama waume kwa wake zao. Mwanzo walianza kama utani, wakifikiri wamepata kama kawaida yao, Lakini wakawa wamepatikana. Kinachowashangaza zaidi ni kwamba wake zao hawatishi sana kwa sura, lakini mbinu za kuwamiliki wanazo.Yaani Sammy na Jeff wamemilikiwa sasa. Hawafurukuti.Na kadiri miaka inavyokwenda, na watoto kuanza kukua ndivyo wanavyozidi kunasa kwenye mtego wa kuwajibika katika jamii. Makusudi ya Mungu yanatimia maishani mwao wapende wasipende. Lakini nini kilichopelekea vijana hawa kuwa kama walivyokuwa? Wenyewe wanasema vituko vya wahubiri Nairobi viliwafanya wasitilie maanani maisha ya utakatifu kama inavyofundisha BIBLIA, na wakaishia kuona kila kitu ni kama maigizo. Wamewahi kufanya kazi ya Mungu karibu na kila mchungaji Nairobi. Kwanza walimsaidia Pius Muiru kuanzisha kanisa Nairobi, na alipopata pesa nyingi ikawa hawawezi kumuona tena. Alijiwekea walinzi wakali kuliko wale wanaomlinda rais na ikawa hawawezi kumuona. Wanasema Mambo yalikuwa mabaya zaidi wakati Muiru alipokubali kuolewa na mama wa makamo aliyekuwa akimsaidia kihuduma. Jeff anasema yeye ndiye aliyekuwa aolewe na huyo mama lakini akaruka mitego yake.Anasema bora alivyo, kuliko kuwa na kila kitu ukose utu na haki maishani. Hata kuoa kwao kulikuwa kwa miujiza.ilikuwa hivi.Mchungaji mmoja kutoka Tanga nchini Tanzania aliwaalika kwenye mkutano wa nje. Kama kawaida yao waliamua kwenda wakiwa wamejihami kwa kila jambo. Walitafuta mabinti wawili kutoka sehemu za mashambani. Safari hii waliwapata wa kabila lao KIKUYU. Waliwaambia kwamba watasafiri kwenda Tanzania, na kwa sababu wachungaji huko huwa wanauliza maswali mengi wanapomuona muhubiri akiwa na mabinti, walikubaliana kwamba wakifika huko wasijali kutambulishwa kama wake zao. Mabinti walikubali haraka kwani ndoto zao zilikuwa kwamba siku moja waitwe hivyo. Safari ilianzia Nairobi kupitia Arusha. Walipofika Arusha iliwabidi walale siku moja. Kipesa hawakuwa sawa sana, iliwabidi wamtafute mchungaji wanayemfahamu Arusha. Walipompata walijitambulisha kama Mr.na Mrs. Mchungaji alipouliza mbona hakualikwa arusini, Jeff alidakia haraka kwamba pengine kadi ya mwaliko ilipotelea kwenye ofisi za Posta Tanzania. Alidai kwamba aliituma, na alishangaa sna kutomuona Mchungaji kwenye arusi yao iliyohudhuriwa na maelfu ya watu.Mchungaji aliguna kidogo, Lakini ilimbidi akubali japo kwa shingo upande. Alipowauliza mabinti kama kweli wote waliolewa siku moja, walionyesha kutojiamini na walipokuwa wakijitizama kwa haya, Sammy aliingilia kati na kusema bado wanaona haya kwa sababu masuala ya kuolewa ni mageni sana kwao. Alisisitiza kwamba kama siyo UTUMISHI WA MUNGU, saa hizi wangekuwa kwenye hoteli moja ya kifahari jijini Nairobi wakiendelea na 'HUNEY MOON yao. Mchungaji alionyesha kuwahurumia, na akawatafutia kila mmoja chumba chake ili kila mtu awe na wakati wa faragha na "mke wake" Pia alihakikisha kwamba amewapa shuka mpya ili malazi yawe matakatifu. Laiti angejua kwamba ndiye anayeibariki ndoa yao kwa mara ya kwanza. Baada ya chakula cha jioni, Mchungaji aliongoza maombi na kuwaruhusu wakajipumzishe. Kwenye maombi yake Mchungaji aliomba hivi. "Mungu Baba tunakushukuru kwa ajili ya wageni. Tuliwajua walipokuwa vijana, na imekupendeza kwamba umewapa wasaidizi watu wa kufanana nao. Ni wewe uliyesema kwamba mtu atamuacha baba yake na mama ili aambatane na mke au mumewe. Tizama watumishi wako hawa kutoka Kenya ambao hawakuona kuoana pamoja na raha zake ni kitu cha dhamana kuliko neno lako, na ndiyo maana wakiwa katika siku zao za mwanzo wa ndoa, wameamua kuja kuifanya kazi yako nchini Tanzania.. Eee Bwana bariki usingizi wao katika nyumba yetu, na Kesho wanapoendelea na safari yao mjini Tanga utawabariki na pia utaubariki mkutano watakaokuwa nao huko. Tunasema asante maana tumeomba machache hayo katika Jina la Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wetu." Na wote waliitikia AMEN. Mchungaji bila kujua, alikuwa amewaoza watu kwa mara ya kwanza. Hata wewe unajua kilichoendelea. Siyo lazima niseme. Asubuhi baada
ya kupata kifungua kinywa, mchungaji wa Arusha ilibidi awasaidie "Watumishi
wa Mungu" nauli ya kuwafikisha Tanga, pamoja na pesa kidogo za
matumizi njiani. Njiani walikuwa wakicheka, Kinadada nao soni zikaanza
kuwaisha usoni. Pengine walianza kufurahia kuitwa"wake."
Kufika Tanga walipokelewa kwa shangwe na wimbo ukawa ni ule ule. Baada
ya mkutano kwisha, Kinadada wa Tanga walionekana kupenda sana kuwa
karibu na "wake wa watumishi wa Mungu Toka Kenya" Maswali
waliyokuwa nayo kuwahusu wasanii hawa machachari waliyaelekeza kwa
"wake zao",Jambo ambalo halikuwapendeza sana Jeff na Sammy.
Uongo walioutunga wenyewe, ukaanza kuwaendea kinyume. Waliwatamani
sana mabinti wa Tanga, lakini "WAKE BANDIA " wakaanza ulinzi
wa kweli. Kila walipojaribu kuutafuta mwanya wa kuwaacha kidogo Hawa
wake waliwaganda kama kupe amgandavyo ngombe. Mbaya zaidi walikuwa
wamewafundisha mbinu za kudanganya wakati wa matatizo. Ikwa wake Bandia
wamepata nafasi ya kuwajua ndani na nje na ikawa ni vigumu sana kudanganywa.
Baada ya mkutano wa Tanga, kile walichofikiria ni kupata, kikawapata.
Mkutano wote ulitangaziwa kwamba Jeff ameoa, na pia Sammy ameoa. Hayawi
hayawi mwisho yakawa. Waliondoka Tanga Mate yakiwatiririka kwa tamaa,
kwani kama wanavyosema wenyewe, watoto huko ni kama wakuchongwa siyo
kuzaliwa. Tena wanadai kwamba wana heshima gunia zima kama siyo debe
zima. Siyo kwamba wanawadharau wake zao, Lakini wanakiri kwamba waliwapata
haraka kwa ajili ya safari na haikuwa ule uchaguzi wao hasa. Walikuwa
wamejiwekea viwango ambavyo wanakiri kwamba wake zao hawana. Pengine
Mungu aliyaona mateso ya mabinti waliodanganywa kwamba wangeolewa
na wasanii hawa bila mafanikio, na akaamua kuwaoza kilazima, au kama
wanavyosema Kenya, Waliozwa KYANGUVU. Waliporudi Nairobi walijaribu
kila mbinu wajinasue wabaki huru, Lakini watoto wa KIKIKUYU walikuwa
na mbinu mmbadala. Waliwashinda maarifa mpaka wote wakapata watoto
na wakawalazimisha kwenda kwa wazazi wao na sasa ni miaka zaidi ya
mitano, na kama bado wana ndoto za kuoa wasahau kwani urefu wa maji
waliyoyaingia ni vigumu sasa kutoka. Inaonekana kwamba wameikubali
hali hata kama ni shingo upande. Umri nao umeanza kuwapiga chenga
kwani sasa hawawezi kumdanganya binti yeyote kwamba wao ni vijana
wa tajiri fulani Nairobi. Vijana gani ambao kichwani nyele zina mvi
moja moja? na kila kukicha zinazidi kuongezeka. Isitoshe watoto wanakua.
Tena wake zao sasa wanazijua mbinu zao zote. GTV tunamshukuru Mungu
aliyewatumia mabinti jasiri wa KIKIKUYU kumaliza kile kilichoonekana
kama tishio la kazi ya Mungu Afrika ya mashariki. Shetani akiwatumia
vijana hao wakati wa ujana wao, wakijua au bila kujua, walikuwa wameharibu
sana USHUHUDA wa Yesu Nairobi na kote walikowahi kutembelea vijana
hao ambao sasa ni wazee wanaoelekea uzeeni. ILa hata sasa wanasema
hawakosekani wanaotaka kujua wenzao walikuwa wakidanganywaje? Ushauri
wetu kwao ni kwamba wala wasiulize. Isije ikawa wanaamsha maroho yaliyolala
kuzimu yaje tena yaanze vituko. Tunawaombea Mungu awape nguvu ili
wakati huu uliobaki maishani mwao wautumie kuliinua Jina la Yesu ambaye
walikuwa wakimrudisha msalabani kwa matendo yao. Pia waitumie nafasi
hiyo kuwakemea wachungaji bandia ambao wanatumia maroho ya kuzimu
kufanya kile kinachoonekana siku hizi kama miujiza. Eti watu watoe
pesa wampe mchungaji, naye awamwagie mafuta ya karanga usoni kama
baraka. Huo ni uongo kutoka kwa shetani mwenyewe na tunaukemea kwa
jina la Yesu USHINDWE. Kabla hujaanza kuwahukumu soma kisa kifuatacho
halafu ujaze mwenyewe. James
Kim Apokonywa mchumba Kanda
Mpya Redio
za Injili na Wanamuziki wa Gospel
Nayo serikali ya Kenya imekuwa ikimfuatilia kwa karibu mchungaji Ng'ang'a baada ya kiongozi wa kundi la Mungiki kudai ameokoka na kujiunga na kanisa la Ng'ang'a. Wanaiona hiyo kama mbinu ya MUNGIKI kuja na sura mpya ya kanisa la Neno Evangelism. Wanaomsaidia kihuduma wanalipwa pesa kidogo sana na hazitoshi kumudu mahitaji yao. Wengi wamehamia katika kanisa la Mchungaji Lai Mombasa kwani anawalipa mara tatu ya wanavyolipwa NENO. Wahudumu wa NENO wengi hulipwa Kshs. 5000 kwa mwezi. Wanapohamia kwa LAI wanalipwa mara tatu ya walivyokuwa wakipokea walipokuwa kwa Ng'an'ga. Japo kila siku sadaka hutolewa zaidi ya Kshs.100,000 lakini kutokana na matumizi mengi mchungaji bado anadai hazitoshi. Maisha ya kifahari, miradi mingi isiyomalizika, imefananishwa na mtu aliyeweka unga kabla maji hayajachemka na anajaribu kusonga ugali. Haijalishi ataongeza moto kiasi gani, lakini ugali huo hauwezi kuiva. Wengine wanamlaumu mchungaji Ng'ang'a kwa kujitakia makuu. Wengi wa washirika wake wanalalamika kwamba matumizi katika kanisa hilo ni ya juu kiasi kwamba hawawezi kuyamudu. Walitoa mfano wa vipindi katika redio na TV. Bei zake ni juu sana kwani kila wiki wanalazimika kulipa KSHS. 70,000 hiyo ni kwa ajili ya vipindi katika vyombo vya habari tu. Pia walisema kila mwezi hulazimika kulipia nyumba ya Mchungaji huko Nyali Mombasa na nyingine Runda Nairobi. Nyumba ya Mombasa ni KSHS 30,000 kila mwezi wakati ile ya Nairobi ni KSHS 40,000 kila mwezi. Walikumbusha kwamba nyumba hizo lazima zilipiwe miezi mitatu mbele. Tena walilalamika kuhusu michango ya kununua gari la mchungaji. Kwa imani mchungaji hupenda kuendesha gari kubwa ya kifahari na ya kisasa kabisa. Kwa sababu kampuni za magari hutoa magari kila kukicha, hakuna siku watamaliza kununua gari la mchungaji. Likitoka jipya mchungaji anasema ataliendesha kwa imani. Imani ya mchungaji inawalazimu washirika waingie mifukoni kuitimiza imani hiyo. Wengi waliokuwa wakuu katika mashirika imewabidi wafutwe kazi baada ya mashirika hayo kupata hasara ya mamilioni ya pesa. Kuna wale wanaosema hasara kwenye mashirika hayo ilisababishwa na ufujaji wa pesa zilizopelekwa kanisani kulipia gharama za juu kanisani ambazo hakuna dalili kwamba zitamalizika karibuni. Ni kweli kila mtu amepewa huduma tofauti na mwingine, lakini tofauti hiyo ikiwa ni kuwalemea washirika na mahitaji ya pesa yasiyoisha, tuna mashaka kama na hiyo ni huduma ya Mungu.
Washirika
Nairobi wa nani? Kundi linalowafadhili wahubiri si watu wengi. Wakiamua kuhama itakuwa vigumu kwa wahubiri kumudu gharama za juu kuendeshea huduma zao.Inasemekana kwamba wahubiri wanaoonekana kwenye TV gharama zao ni Kshs.500,000 kwa juma moja. Sasa matajiri wazito wakihama kama walivyomhama Muiru, Sishangai kumsikia akisema kwenye TV kwamba Bwana amemwonyesha kwamba yule mtu ambaye kanisa limejengwa kwenye shamba lake, asarende hati za kumiliki shamba hilo kwake mara moja, kwani hiyo ni amri kutoka juu kwa Mungu mwenyewe. Wengi walishitushwa na kauli hiyo na wakabaki wakijiuliza nini kitafuatia baada ya kusarenda hati za kumiliki mashamba? Pengine kitakachofuata ni kusarenda wake zetu kwa wahubiri. Mungu asaidie tusifike hapo, lakini kila dalili zinaonyesha tunaelekea hapo. Maisha ya hali ya juu yamewalewesha wahubiri na hawataki kushuka. Lakini Mungu atawashusha. Wengine wamefikia hatua ya kujitengenezea kile watakachokiita miujiza kwenye TV. Wanachaguliwa watu watakaosema kwamba wamepona ili kuvuta umati kanisani. Wakija wasipone, wanaondoka kimya kimya. Kwa sababu TV bado inatumika kuwatapeli, kila siku hawakosi watu wapya. Wanakamuliwa, wakikauka wataondoka wapishe wengine. Yaani mtindo wa makanisa umegeuzwa na kuwa kama gari la abiria. Linabeba likishusha na hakuna abiria wanaoweza kusema gari ni lao. Makanisa nayo hivyo hivyo yamekuwa ni mali ya wachungaji na familia zao. Washirika hawana lao. Wanachopata ni mafundisho yenye chumvi nyingi, ikiwashinda kumeza, wanaambiwa wameze kwa lazima ya Mungu. Wanatoa na hawaruhusiwi kuuliza pesa hizo zinatumika vipi. Yani Kanisa ni kama KIOSK ya Mchungaji. Anafungua KIOSK asubuhi saa kumi na mbili. Wanaingia kwa maombi ya asubuhi, maarufu kama "Morning Glory" Sadaka asubuhi lazima watoe. Mchana wanakuja maombi ya mchana maarufu kama "Lunch Time Meeting" Hapo pia wataahidiwa ahadi za baraka kutoka kwa Mungu, lakini wao wanapaswa kumbariki Mchungaji wao anunue BENZ ya milioni kumi na tano. Jioni bado watakuja kuombewa baraka pamoja na kupakwa mafuta, kisha wataulizwa kutoa ili kiwanja cha kanisa kinunuliwe. Bei ya kiwanja wataambiwa ni milioni 30 pesa za Kenya. Kila mtu atatoa mpaka akose nauli ya matatu kurudi wanakoishi. Usijali kama kweli kuna kiwanja kinachonunuliwa, au pesa hizo zinatumika kujenga nyumba ya kibinafsi ya mchungaji katika mtaa wa Karen, na hata kama kiwanja kikinunuliwa, na tuna mashaka kama kitanunuliwa, kitakuwa kimesajiliwa kwa jina la mchungaji na siyo Kanisa. Hata washirika wakiamua kumtimua Mchungaji, Hawawezi kulipa madeni ya mamilioni ya shilingi kanisa linayodaiwa na vyombo vya habari ambavyo hurusha vipindi vya mchungaji huyo. Watajiuliza mbona tunachangishwa kila siku kulipia vipindi? Kumbe kwa makusudi Mchungaji halipii vipindi hivyo ili kuwazuia washirika wasije wakawaza kumtimua wachukue usukani Kanisani hapo. Kwa Mchungaji mkimtimua atachukua mkoba wake aondoke awaachie kiwanja ambacho siyo mali yenu, Tena hakuna dalili zozote kuonyesha kwamba kiwanja husika kinatarajiwa kuwa mali ya kanisa, Nadhani wengi watazimia kuambiwa kwamba kiwanja hicho hakijalipiwa chochote. NI ugumu huo ndio unaowafanya washirika wakose nguvu ya kudai haki zao. Nasi tunauliza. Mpaka lini wahubiri matapeli wataruhusiwa kuwaibia watu mchana machoni pa Serikali na kila mtu?
Wamasai wanaohubiri
kwenye Redio Biblia Husema maarufu kama Shonara Ole Tiambati
na Samiet Ole Leteipan wameigiza kipindi "Hakuna nuru gizani"
Bonyeza hapa chini usikize kipindi. Lakini hii haiwapi haki serikali ya sasa kulibomoa kanisa la MAXMAM MIRACLE CENTRE. Pamoja na kwamba Muiru amekiri kutokuwa na hati ya kumiliki eneo lilipojengwa kanisa, kama walipata kihalali hakuna mwenye haki ya kuwanyanganya kwa kisingizio cha barabara. Picha inaonyesha wazi kwamba barabara ziko mbili na kuna nafasi kubwa katikati na pembeni kuiongeza barabara husika bila kuharibu mali za raia na hasa makanisa ambayo ni mahali pa kumwabudu Mungu. Dunia na Vyote ni mali ya Mungu. Inashangaza kuona kwamba ili wahubiri wapatiwe sehemu za kujenga makanisa, lazima wajipendekeze kwa wanasiasa. Tatizo ni wakati wanasiasa wanapotolewa madarakani na wengine kuingia. Dunia ya Mungu chini ya sheria za wanasiasa. Mpaka lini tutaendelea kunyanyaswa kwenye dunia ya muumba wetu? Hivi kweli sehemu za kuabudia zinaweza adimika kiasi ni lazima tuwapigie magoti wanasiasa? Wao waliumba dunia gani mpaka kibali cha kujenga mahali pa kuabudia watoe wao? Hatupingani nao, ila wafanye waonavyo ni vyema. Lakini wajue Mungu mwenye dunia na kila kitu mpaka maisha yao anawatizama. Hawawezi kutudanganya kwamba tuna UHURU wa KUABUDU wakati kupata sehemu ya kuabudia ni kitendawili. Sheria hutungwa na watu kwa ajili ya watu. Sheria zinapotumika kuwabomolea watu mali zao, ni wakati wa watu kutunga sheria nyingine za kuwajengea watu mali zao. Amri za Mungu hazibadiliki kwani hazina makosa. Sheria za wanadamu zinatakiwa zibadilishwe kila mara kwani wanadamu wana makosa mengi. Nini kinachowafanya mfikiri kwamba sheria za sasa hazina makosa?
KWAMBA TAFSIRI YA SHERIA INAWEZA PINDISHWA ILI IWAADHIBU WANAOTAKIWA
KUADHIBIWA NAYO HILO NDILO LINALOTUPA MASHAKA. JE! NIA YA SERIKALI
NI KWELI KULINDA SHERIA NA UTENGAMANO AU KUWATAFUTA WALIOIUNGA
MKONO SERIKALI YA AWALI ILI WAADHIBIWE. SERIKALI YA SASA INATAKA
KUUNGWA MKONO. JE INATAKA WANAOWAUNGA MKONO SASA NAO WAJE WAADHIBIWE
NA SERIKALI IJAYO? AU WATATAWALA MILELE? KILA LA KHERI.
Tuma picha na maelezo kwa munishi@munishi.com ![]() http://munishi.com FREE! Send photo and information to munishi@munishi.com
Redio
Injili FM Hii ni redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com Yesu ni nuru ya ulimwengu, Alikuja tutoke gizani. Giza na nuru hazikai pamoja. Yaani hakuna nuru gizani. Mungu anakupenda jinsi ulivyo. Ukimwamini na kutubu makosa yako utaokoka. Huwezi kuokoka ndipo uamini baadae. Hapana. Kwanza unaamini, kisha unatubu, na ndipo Mungu anakusamehe na kukupa uwezo wa kufanyika mwana wa Mungu. Uwezo wa Mungu ndani yako ndio wokovu. Unaendelea kuisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com Ukisha pokea msamaha wa dhambi, omba lolote kwa Mungu na maombi yako yatajibiwa. Katikati yako na Mungu ni Yesu peke yake. Siyo Mchungaji wala Askofu. Omba mwenyewe kwa jina la Yesu, na Mungu atakujibu maombi yako. Baraka za Mungu hazinunuliwi kwa pesa. Huwezi kumhonga Mungu ndipo akubariki. Mungu ni tegemeo letu sote. Wachungaji na washirika, tunatakiwa kumtegemea Mungu kwa baraka zetu. Siyo wachungaji wawategemee washirika kwa baraka zao, huku wakiwaambia washirika wamtegemee Mungu. Nani walio katika nafasi nzuri zaidi kumtegemea Mungu? Unaendelea kuisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com Je baraka
za Mungu zinawezaje kumpita mchungaji ziwaendee washirika ili
washirika wambariki mchungaji? Siku hizi washirika wanawinda
baraka zao kutoka kwa wachungaji, Wanasahau kwamba hata wachungaji
wanawinda baraka zao kutoka kwa washirika. Wanajiunga na makanisa
yaliyovuma ambayo wachungaji wake wanatembelea magari makubwa
na kuishi kwenye mitaa ya kifahari. Lengo ni ili na wao wafanikiwe
kimaisha. Wakifika wanashangaa kukuta mchungaji anawategemea
ili wayalipie maisha yake ya kifahari. Walienda kutafuta mafanikio,
wanarudi wakiwa masikini kuliko walivyokuwa. Walikosea lengo.
Tunatakiwa kumtafuta Mungu kwanza, na hayo mengine tutazidishiwa.
Hiyo ndiyo INJILI. Jiunge na kanisa kwa lengo la kuutafuta uhusiano
wako na Mungu. Usijali kama kanisa hilo lina watu wengi au la.
Nani alikudanganya kwamba wengi hawawezi kuwa wamepotea njia?
Jiunge na wale wanaomtafuta Mungu kwa moyo wao wote hata kama
ni wachache. Sikiliza
sauti yake UPONYAJI Unaisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com Hujambo msikilizaji. Tunamshukuru Mungu kwa ulinzi wake maishani mwetu. Ndiyo maana tunamtukuza na kumwabudu siku zote. Shetani ni muongo. Lazima tupambane naye kila iitwapo leo. Anatumia kila mbinu kuwapotosha watu wa Mungu, Lakini Bwana Yesu asifiwe kwani tumezigundua hila zake. Alifikiri akiwatumia wale wanaojiita wahubiri hatutamgundua. Alijidanganya. Tunajua kwamba yeye huweza kujigeuza na kuwa kama malaika wa nuru. Hatujali atatumia nani, lakini tukiziona dalili zake popote na kwa yeyote tutamkemea arudi kuzimu. Unaendelea kuisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com Kifo cha Yesu msalabani na hatimaye kufufuka siku ya tatu kilimaanisha mengi kwetu tunaomwamini. Sasa tunapokea msamaha wa dhambi, Wokovu wa roho, Uponyaji wa mwili, na baraka maishani Bure. Mtu asikufanyie sarakasi, mbembwe, vitimbi, eti akusukume uanguke ndipo upokee uponyaji. Injili ya Yesu inasimamisha haiangushi. Shetani kazi yake ni kuangusha kwani mwenyewe alianguka kitambo. Ukiona mahali watu wanaombewa na kuanguka anguka hovyo ujue shetani ana mkono wake hapo. Kama nguvu za Mungu ndizo zinazowaangusha, mbona mhubiri huwa haanguki? Unaendelea kuisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com Wengine wanasema wanafanya miujiza kumpita Yesu. Sawa. Je kiutakatifu pia wamempita Yesu? Nina mashaka kama hata wanamkaribia.Hii ni mbinu ya shetani kuongeza chumvi kwenye injili. Tunaikemea katika jina la Yesu ishindwe. Ndiyo ninaamini kwamba Yesu anaponya. Tatizo langu ni watu wanaotumia uponyaji wa Mungu kujinufaisha kibinafsi. Mungu ndiye anayeponya na siyo mhubiri. Uponyaji wako unategeme Mungu na wewe kuliko mhubiri. Hata kama ana nguvu za kuangusha watu, na pengine siyo nguvu za Mungu, haina maana kwamba wewe utapona kwa kuitumia imani yake. Haiwezekani. Kama hujaisikia injili vya kutosha imani yako ijengeke, hata ukiangushwa mara ngapi. Haitaleta tofauti yeyote. Utaangushwa uanguke, ukiamka utakuwa umepoteza pochi na viatu, lakini bado utakuwa mgojwa kuliko mwanzo. Ukimuuliza huyo mhubiri wa vituko, mbona hujapona, utaambiwa kwamba hujatoa fungu la kumi. Utauza gari na shamba ulete pesa zote kwa mhubiri huyo tapeli, lakini bado hali yako itazidi kuwa mbaya. Ni mpaka uijue kweli ya Injili ndipo utawekwa huru. Kweli inasema kwamba kwa kupigwa kwa Yesu wewe ni mzima. Siyo kwa kuangushwa chini. Pole sana. Unaendelea kuisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com Yesu katika
mahubiri yake hakufanya maonyesho tunayoyaona na wahubiri leo.
Alihubiri na kufundisha kweli ya Mungu, walioamini walimwendea
ili awaponye, aliwaambia wapokee kadiri ya imani zao.Yesu hakuwahi
kuwaombea wagonjwa wakakosa kupokea uponyaji wao. Tena Yesu
hakutumia imani yake kuwaponya wagonjwa. Kila mara aliwauliza
waliomwendea kama wanaamini anaweza kuwatendea wanayohitaji.
Walipojibu ndiyo, aliwaambia wapokee kadiri ya imani zao. Leo
hii wahubiri wanawaita wagonjwa waje wawaombee siyo wawahubiriwe
injili. Ndiyo maana wengi hawaponi. Huwezi kupona kwa kuitegemea
imani ya mhubiri.Unatakiwa uwe na imani yako. Imani kwako itakuja
baada ya kusikia Neno la Mungu. Unataka mafundisho ya injili
uijue kweli ikuweke huru. Wacha kuwa na imani tegemezi kwa wahubiri.
Imani zetu zinatakiwa kumtegemea Mungu pekee. Ukiiamini Injili,
Utubu usamehewe, halafu Mungu akupe uwezo wa kufanyika mwana
wa Mungu, Huwezi kuangushwa kwa madai kwamba unaombewa. Utamuomba
Mungu kwa imani yako, na Mungu atakuponya. Soma neno la Mungu
kila siku, kwani ndilo litakalokujenga kiimani. Imani yako ikikua,
utawaona wengine wakiangushwa na kudanganywa lakini wewe utasimama
imara. Yesu alipomfufua Lazaro ilibidi atumie imani yake kwani
Lazaro hakuwa hai kuamini. Wewe uko hai. Imani yako inahitajika
sana katika kusababisha muujiza wako. Sikiliza
sauti yake Wimbo
mpya CCM imewatesa wengi MASAI:
Hakuna Nuru Gizani!! Washirika
Nairobi wa nani? Kundi linalowafadhili wahubiri si watu wengi. Wakiamua kuhama itakuwa vigumu kwa wahubiri kumudu gharama za juu kuendeshea huduma zao.Inasemekana kwamba wahubiri wanaoonekana kwenye TV gharama zao ni Kshs.500,000 kwa juma moja. Sasa matajiri wazito wakihama kama walivyomhama Muiru, Sishangai kumsikia akisema kwenye TV kwamba Bwana amemwonyesha kwamba yule mtu ambaye kanisa limejengwa kwenye shamba lake, asarende hati za kumiliki shamba hilo kwake mara moja, kwani hiyo ni amri kutoka juu kwa Mungu mwenyewe. Wengi walishitushwa na kauli hiyo na wakabaki wakijiuliza nini kitafuatia baada ya kusarenda hati za kumiliki mashamba? Pengine kitakachofuata ni kusarenda wake zetu kwa wahubiri. Mungu asaidie tusifike hapo, lakini kila dalili zinaonyesha tunaelekea hapo. Maisha ya hali ya juu yamewalewesha wahubiri na hawataki kushuka. Lakini Mungu atawashusha. Wengine wamefikia hatua ya kujitengenezea kile watakachokiita miujiza kwenye TV. Wanachaguliwa watu watakaosema kwamba wamepona ili kuvuta umati kanisani. Wakija wasipone, wanaondoka kimya kimya. Kwa sababu TV bado inatumika kuwatapeli, kila siku hawakosi watu wapya. Wanakamuliwa, wakikauka wataondoka wapishe wengine. Yaani mtindo wa makanisa umegeuzwa na kuwa kama gari la abiria. Linabeba likishusha na hakuna abiria wanaoweza kusema gari ni lao. Makanisa nayo hivyo hivyo yamekuwa ni mali ya wachungaji na familia zao. Washirika hawana lao. Wanachopata ni mafundisho yenye chumvi nyingi, ikiwashinda kumeza, wanaambiwa wameze kwa lazima ya Mungu. Wanatoa na hawaruhusiwi kuuliza pesa hizo zinatumika vipi. Yani Kanisa ni kama KIOSK ya Mchungaji. Anafungua KIOSK asubuhi saa kumi na mbili. Wanaingia kwa maombi ya asubuhi, maarufu kama "Morning Glory" Sadaka asubuhi lazima watoe. Mchana wanakuja maombi ya mchana maarufu kama "Lunch Time Meeting" Hapo pia wataahidiwa ahadi za baraka kutoka kwa Mungu, lakini wao wanapaswa kumbariki Mchungaji wao anunue BENZ ya milioni kumi na tano. Jioni bado watakuja kuombewa baraka pamoja na kupakwa mafuta, kisha wataulizwa kutoa ili kiwanja cha kanisa kinunuliwe. Bei ya kiwanja wataambiwa ni milioni 30 pesa za Kenya. Kila mtu atatoa mpaka akose nauli ya matatu kurudi wanakoishi. Usijali kama kweli kuna kiwanja kinachonunuliwa, au pesa hizo zinatumika kujenga nyumba ya kibinafsi ya mchungaji katika mtaa wa Karen, na hata kama kiwanja kikinunuliwa, na tuna mashaka kama kitanunuliwa, kitakuwa kimesajiliwa kwa jina la mchungaji na siyo Kanisa. Hata washirika wakiamua kumtimua Mchungaji, Hawawezi kulipa madeni ya mamilioni ya shilingi kanisa linayodaiwa na vyombo vya habari ambavyo hurusha vipindi vya mchungaji huyo. Watajiuliza mbona tunachangishwa kila siku kulipia vipindi? Kumbe kwa makusudi Mchungaji halipii vipindi hivyo ili kuwazuia washirika wasije wakawaza kumtimua wachukue usukani Kanisani hapo. Kwa Mchungaji mkimtimua atachukua mkoba wake aondoke awaachie kiwanja ambacho siyo mali yenu, Tena hakuna dalili zozote kuonyesha kwamba kiwanja husika kinatarajiwa kuwa mali ya kanisa, Nadhani wengi watazimia kuambiwa kwamba kiwanja hicho hakijalipiwa chochote. NI ugumu huo ndio unaowafanya washirika wakose nguvu ya kudai haki zao. Nasi tunauliza. Mpaka lini wahubiri matapeli wataruhusiwa kuwaibia watu mchana machoni pa Serikali na kila mtu?
Bonyeza
hapa usome zaidi
Waruinge
Atawazwa Uchungaji Komba
Ajikomba na CCM
Gospel Television Moto wa kuotea mbali
Ikiwa ndio kwanza inajitayarisha kurusha matangazo yake, GTV imekuwa tishio kwa Serikali Tanzania. Aliyekuwa Rais wa kimabavu nchini humo William Benjamin Mkapa aliamuru polisi wawatie mbaroni wote watakaopatikana na VCD za GTV. Kisa ni kwamba Gospel Television ilikuwa imezungumzia uwezekano wa Mkapa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kutumia madaraka vibaya. GTV ilikuwa imedai kwamba, Mkapa akiwa madarakani aliwaamuru POLISI wawaue Wazanzibari zaidi ya 70 kwa kosa la kusema CCM Chama Cha Majambazi hawakitaki. Pamoja na mambo mengine GTV ilipendekeza tume ya kumchunguza Mkapa iundwe na akipatikana na makosa sheria ichukue mkondo wake. Pia GTV ilidai kwamba Mkapa aliitawala Tanzania kama mali yake binafsi kwani hakutaka ushauri wa mtu yeyote. Bado msimamo wa GTV ni huo na hatuombi msamaha kwa Mkapa wala CCM. Habari Zaidi Hotuba ya Munishi kwa TAIFA
![]() ![]() ![]() ![]() ![]() ![]()
![]() ![]() ![]()
|
||||||||||||||||||||||||||||||
|
|
|
|