Kibaki ajenga Hospitali ya kisasa
Nairobi

Dr.
Dan Gikonyo na mkewe Betty, mbele ya hospitali ya kisasa iliyojengwa
katika mtaa wa Karen Nairobi. Dr. Gikonyo ni daktari binafsi wa
Rais wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki. Hospitali hiyo yenye mitambo
ya kisasa, inasadikiwa kuwa ya kipekee Afrika. Inaweza kufanya mambo
mengi ambayo viongozi wa Afrika hulazimika kwenda ngambo kutibiwa.
Kwamba Kibaki alifikiria kujenga hospitali kama hiyo Kenya, ni hatua
inayostahili kupongezwa. Lakini gharama za matibabu katika hospitali
hiyo ni za juu kiasi kwamba matajiri tu ndio watakaoweza kumudu.
Itambidi Kibaki afikirie jinsi ya kuiboresha hospitali ya Kenyatta
ambayo ndiyo hospitali ya rufaa nchini Kenya ili wananchi wa kawaida
waweze kumudu gharama za matibabu. Vinginevyo itaonekana kwamba
matajiri pekee ndio wanaostahili kuishi Kenya, na wengine wapotelee
mbali.

Mitambo ya kisasa
ndani ya hospitali mpya ya Kibaki. Kupimwa shinikizo la damu kisha
ulazwe hapo wiki moja, ujue shamba na gari pamoja na akiba yako
yote imekwisha. Omba Mungu azidi kukulinda na akupe afya njema kwani
huwezi kumudu gharama za hapa. Ila pia jifariji kwamba hata hao
wenye uwezo wa kutibiwa hapo, hufika mahali mitambo hiyo ikashindwa
kuwasaidia na ikifikia hapo inawabidi wakubali kwamba Mungu pekee
ndiye anayeweza kulinda afya zetu. Siyo vibaya wenye pesa wakijaribu
bahati ya kujiweka hai wazifurahie pesa zao ulimwenguni. Lakini
kwa muda gani?

Aliyekuwa Makamu wa kwanza wa rais Tanzania Mzee Kawawa akielekezwa
kwenye Wadi kulazwa. (Lakini siyo katika Hospitali mpya ya Kibaki
, bali Muhimbili Dar es Salaam. Pengine wajifunze kwa Kibaki waboreshe
Muhimbili ifikie kiwango cha hospitali ya Kibaki Nairobi) Inasemekana
anasumbuliwa na mifupa. Yeye na Nyerere ndio waasisi wa siasa ya
Ujamaa Tanzania. Inasemekana Kawawa katika kuitekeleza siasa ya
Ujamaa, alisababisha vifo vya mamia ya Watanzania pale alipowahamisha
makwao na kuwapeleka msituni ambapo vijiji vya Ujamaa vilitarajiwa
kujengwa.Watanzania wengi wakati huo walipoteza maisha yao kwa kuliwa
na wanyama pori. Na wengi walikufa kwa njaa pamoja na magonjwa yaliyosababishwa
na kurundikwa mahali pamoja msituni bila maji wala matibabu.