


.com

TV ya INJILI Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM
Tel.
254722602445 E-mail:
munishigtv@gmail.com or munishi@gospelgtv.com
Matukio
FaceBook








TVT NI TV YA TAIFA
AU YA CCM?

Wanahabari Tanzania,
hasa wale wanaofanya kazi katika vyombo habari vya serikali, ni vibaraka
wa serikali. Wanaegemea upande wa serikali hata kama serikali husika
inakiuka haki za binadamu. Tangu enzi za Nyerere vyombo vya habari
Tanzania viligeuzwa kuwa wasemaji wa serikali. Nyerere aliitumia sana
redio Tanzania Dar es Salaam kueneza injili yake ya ujamaa na kujitegemea.
Matokeo yake yakawa ni kushindwa vibaya kwa siasa ya ujamaa jambo
lililopelekea afya ya Nyerere kuzorota na hatimaye kuiaga dunia. Soma
Zaidi





Mbunge wa CCM (viti maalum) Bi Amina Chifupa
akanusha kwamba amemuacha mumewe Bwana Mohamed Mpakanjia, na kuwa
kimada wa Rais Kikwete. Alisema wanaoeneza uvumi huo wana nia ya kumwaribia
ndoa yake. Hii ni kufuatia taarifa ya vyombo vya habari kwamba mbunge
huyo sasa ana nguvu kuliko Rais mwenyewe. Cha ajabu ameanza kuwapa
tumbo joto hata wabunge wenzake kutoka chama tawala. Usijali kwamba
hakuchaguliwa na wananchi, Lakini aliyemteua bungeni alijua kwa nini
alifanya hivyo. Pengine ni kwa sababu ya dini yake, au urembo wake,
na kuna wale wanaoenda zaidi na kusema ni kwa sababu ya misimamo yake
katika masuala ya kijamii.Vyovyote vile, lakini sisi tunasema adui
wa adui yako ni rafiki.Soma
Zaidi
Bishop Ndzomba afungua makazi
ya watoto yatima
SUSTAINABLE
SOLUTION FOR THE KENYAN ORPHANS.

Bishop Robert Mdzomba afungua kituo
cha watoto yatima Kenya. Asema ni uvumbuzi wa kudumu kwa wale wasiobahatika
katika jamii. Atoa mwito kwa wahisani wauchangie mradi huo kwa moyo
wa kuwajali wengine. HABARI
ZAIDI
Kiboro ametoka Nation yakarabatiwa

Gazeti la Nation kwa mara nyingine
wamegeuza sura, Baada ya mkurugenzi wa zamani bwana Wilfred Kiboro
kunyeshwa mlango. Mkurugenzi mpya amekuja na mbinu mpya. Ana kibarua
kizito kurudisha heshima ya Nation kama gazeti linalozingatia maadili
ya taaluma ya uandishi habari Soma
Zaidi

"CCM Wakiniua Mnizike Kenya"Asema Munishi
Msafara
wa Moi ajalini

Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Daniel
Toroitich Moi, akiuguza majeraha aliyoyapata kwenye ajali iliyohusisha
msafara wake, lakini gari iliyogongwa ni ile iliyokuwa imembeba yeye.Maswali
mengi yameulizwa, lakini majibu yake yatatoka kwa mkuu wa Polisi.
Iweje gari iliyombeba RAIS igongwe wakati zile za walinzi ndizo zilizopaswa
kugongwa zikimlinda RAIS? Je lilikuwa jaribio la kuyakatiza maisha
ya Moi? Kibaki Rais wa sasa Kenya analionaje hilo? Marekebisho gani
serikali itayafanya katika kikosi kinachomlinda Rais wa zamani? Kuna
mtu atakayefutwa kazi kufuatia ajali hiyo? Habari
zaidi
Kibaki
achaguliwe tena?
Machozi ya Uhuru

Kiongozi wa Upinzani Kenya Bwana Uhuru
Kenyata akilia machozi ya Uhuru
Tatizo la wachuuzi halitafutiwi dawa makusudi. Wanasiasa huwatumia
wachuuzi wakati wa uchaguzi.Wengi wa wapiga kura katika nchi za Afrika
ni masikini wanaojitafutia riziki kwa njia za kuchuuza biashara ndogondogo.
Siyo dhambi kufanya hivyo. Wafanyibiashara wakubwa huanza kwa kuchuuza
kwanza. Kwamba wanasiasa watawaamuru polisi wawamiminie wachuuzi risasi
za moto vichwani, hilo linatisha. Sambamba na hilo, hatuungi mkono
hatua ya wachuuzi kulipiza kisasi kwa kumuua askari polisi. Wote wamekuwa
wauaji. Lakini haiingii akilini kuona polisi wa kenya wakiwaua raia
wa Kenya kwa kosa la kujitafutia riziki zao za kila siku. Hata kama
Nairobi inatakiwa kuwa safi, lazima usafi huo uwe wa kiwango cha nchi
changa za kiafrika ambazo umasikini uko kwa kiwango cha kutisha. Kuigiza
usafi wa miji ya nchi zilizoendelea, kutaigawa nchi katika matabaka
ya matajiri wachache wasiotaka kuona masikini karibu nao. Tunaomba
isifikie mahali pa kutungwa sheria inayosema kuwa masikini ni kosa
linalopaswa kuadhibiwa kwa kupigwa risasi kichwani au kifuani? Habari
Zaidi
Gharama ya kuwa na gari Nairobi

Siku hizi ukifanya kosa barabarani, utakutana na
hawa jamaa. Watakupiga, halafu wataamua wakushitaki kwa kosa gani,
na kisha upelekwe mahakamani kama hutaongea lugha wanayoijua.
Kabla
uamue kununua gari Nairobi, Siyo vibaya ukajifahamisha unatakiwa kuilipia
kiasi gani kwa siku. Kwanza kupata mahali pa kuliegesha lazima umlipe
atakayekuonyesha mahali hapo KSHS 30 na kuendelea. Kisha askari wa
tume ya jiji naye utamlipa KSHS 70 kila siku na ninasikia gharama
hiyo itaongezeka kufikia KSHS 200 kwa siku. Ukifikiri umemaliza kulipa,
bado unatakiwa ulipe KSHS 50 na kuendelea kwa mlinzi atakayekulindia
taa za gari lako pamoja na vibandiko vinavyoonyesha gari yako ni aina
gani zisingolewe. Ukipuuzia, yeye huyo huyo ndiye atakayefanya mpango
gari yako iwe haina vibandiko kwenye magurudumu, au taa za kuonyeshea
ishara utazikuta hazipo. Ukifikiri yataishia hapo, kuna yule atakaekuombea
nafasi kwa wenye magari wakupe nafasi ya kutoka ulipoliegesha gari
lako. Huyo hupokea chochote. Sasa unaweza kuelekea nyumbani, na ni
kama hukufanya kosa lolote la trafiki ukamatwe. Kama utakuwa umekamatwa
basi kiwango unachotakiwa kubeba kwa siku siyo chini ya KSHS 20,000
ili uwe salama pande zote. Ukikosa kiwango hicho, usishangae siku
moja utakosa kurudi nyumbani, na watakapokutafuta hospitalini wakukose,
tena wakutafute chumba cha maiti wakukose, basi wakienda jela watakukuta
umefungwa miezi miwili au mitatu kwa kosa la wewe kuwa na gari bila
kubeba KSHS 20,000 kila siku kukufanya uwe salama. Na hapo ni kama
hujagonga Benzi ya mtu nyuma uvunje taa moja tu ya nyuma. Kama gari
yako ni kama yangu, basi itauzwa, na bado haitatosha kuilipa taa moja
ya Benz. Pole nimesahau mafuta ya petroli na Oil na mafundi kama itaamua
kukataa kunguruma kwa sababu zozote. ZAIDI

Kikwete Ameanza
wizi
Anaendeleza mbinu za Nyerere kuwatisha
raia
Miezi
mitatu madarakani, Kikwete ameanza kutumia mbinu za Nyerere kuwatisha
raia Tanzania. Anawatuhumu wananchi kwamba mali walizo nazo hawakuzipata
kihalali. Hii ni mbinu ya Serikali kuhakikisha mali zote Tanzania
ziko mikononi mwa watu wanaodhaniwa siyo tishio kwa CCM. Ni zoezi
la kisiasa kukiimarisha chama tawala. Kwamba Kikwete anatumia mbinu
hizo wakati huu, inashangaza. Nchini Tanzania wenye mali kihalali
ni wanachama wa CCM na viongozi wake. Wengine wote hata kama siyo
wanachama wa chama chochote cha kisiasa, wakiwa na mali CCM hawalali
usingizi. Watatunga mbinu za kuwaita majambazi wakati wenyewe ni majambazi
nambari wani.
Kibaki ajenga Hospitali ya kisasa
Nairobi

Dr. Dan Gikonyo na mkewe Betty, mbele ya hospitali ya kisasa iliyojengwa
katika mtaa wa Karen Nairobi. Dr. Gikonyo ni daktari binafsi wa
Rais wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki. Hospitali hiyo yenye mitambo
ya kisasa, inasadikiwa kuwa ya kipekee Afrika. Inaweza kufanya mambo
mengi ambayo viongozi wa Afrika hulazimika kwenda ngambo kutibiwa.
Kwamba Kibaki alifikiria kujenga hospitali kama hiyo Kenya, ni hatua
inayostahili kupongezwa. Lakini gharama za matibabu katika hospitali
hiyo ni za juu kiasi kwamba matajiri tu ndio watakaoweza kumudu.
Itambidi Kibaki afikirie jinsi ya kuiboresha hospitali ya Kenyatta
ambayo ndiyo hospitali ya rufaa nchini Kenya ili wananchi wa kawaida
waweze kumudu gharama za matibabu. Vinginevyo itaonekana kwamba
matajiri pekee ndio wanaostahili kuishi Kenya, na wengine wapotelee
mbali. Zaidi
Nyumba
yaporomoka Nairobi
Back
to School But...
Anaitwa Ruth Wanjiru. Anamlilia mama asimwache Shuleni. Mpiga picha
BONIFACE MWANGI alipokuwa katika ziara ya shule za Nairobi, alimkuta
Ruth akijigaragaza chini akilia.Kwake, ni nani kama mama? Japo jina
la Shule ni GLAD TOTO NURSERY SCHOOL, ikimaanisha toto lenye furaha,
Wanjiru alionekana kutokuwa na furaha siku yake ya kwanza Shuleni hapo.
Sababu ni kwamba kuna watu walioamua kumtoa nyumbani na kumpeleka shuleni
bila matakwa yake. Haijalishi wazazi wanapenda kiasi gani watoto wao
waende shule, Lakini kama watoto wenyewe hawajui maana ya shule, watakuwepo
kuwaridhisha wazazi, na elimu ya kweli wataipata watakapohitaji au watakapolazimishwa
na hali ya maisha. Je tuwaache watoto mpaka watakapoiona maana ya elimu
ndipo tuwapeleke Shule?
Habari
Zaidi
Kikwete
Azimia
Azimia
Jangwani kwenye mkutano wa lala salama, Magazeti yaandika ana UKIMWI,
Wengine wasema Mwisho umeifikia CCM. Wengine wasema ni Mkono wa Mungu
kuwafundisha adabu CCM
Walikuwa
wakimsikiliza Kikwete kwa makini. Uwanja ni Jangwani jijini Dar. Ilikuwa
siku moja kabla ya uchaguzi. Akiwa katikati ya hotuba yake iliyokuwa
ikirushwa moja kwa moja kwenye TV na Redio Tanzania, Kikwete aliomba
maji. Kabla ayafikishe mdomoni, magoti yalililegea na kuuacha mwili
wa Kikwete kupigiza chini kama nyani aliyekosea tawi. Mkapa na walinzi
wa kikwete walipigwa na butwaa kiasi cha kubaki midomo wazi. Umati ulionekana
kuchanganyikiwa wasijue cha kufanya. Walinzi walikurupuka kumkimbilia
Kikwete ambaye tayari alikuwa chini. Waliwaamuru wapiga picha waelekeze
kamera zao kwa wananchi wakihofia kwamba Rais mtarajiwa ameiaga dunia.
ITV kibaraka wa CCM walikatiza matangazo yao. TVT TV ya Propaganda za
CCM nayo haikuwa na jinsi ila kuwatangazia watazamaji kwamba Kikwete
alikuwa mzima na wasiwe na wasi wasi. Bila kujua kwamba matamshi hayo
ndiyo yaliyowapa watanzania wasiwasi. Hata Kikwete alipoongea masaa
mawili baadaye, watu hawakuamini ni yeye. Ndiyo maana wana CCM wengi
hawakujitokeza kupiga kura wakihofu watakuwa wakichagua kivuli na siyo
Kikwete. Kwa sasa mtizamo wa Watanzania ni kwenye AFYA ya Kikwete. Je
ni mgonjwa kama ilivyodhaniwa?
Habari
Zaidi


KIBAKI AJICHIMBIA KABURI KISIASA
Kosa
la Simba kumwachia fisi windo lake
WAKENYA
WASEMA NO KWA KATIBA KIELELEZO- PIGO KWA KIBAKI

Wahenga zamani
walisema, Simba ni mwindaji hodari.Akifanya kosa la kumwachia fisi
windo lake, Basi mafisi wataitana kwa kicheko, na kabla simba ajue
nini kinaendelea, wingi wa fisi utamzuia kujaribu kudai windo lake.
Pengine arudi msituni akawinde, au afe njaa. Kusema ajaribu kunyakua
windo mdomoni mwa fisi, atahatarisha maisha yake. Isitoshe mabaki
aliyoacha fisi, hayafai kuliwa na yeyote.Mfupa uliomshinda FISI hata
simba hauwezi. Bora akawinde. Inaonekana Raila ameamua kuwinda na
tayari amepata. Kama kawaida KUNGURU Fisi na Mbwa mwitu wanajiandaa
kujaribu bahati yao ili wapewe ngaa mnofu kidogo.Swali ambalo wengi
wanajiuliza ni je safari hii atakubali kuachia windo lake kwa yeyote?
Tunasubiri tuone.Habari
zaidi
Mchungaji Alaani Mauaji Zanzibar

Mchungaji Mmasi wa TAG Kibosho Moshi nchini Tanzania, Amelaani vikali
mauaji ya kisiasa yaliyofanyika Zanzibar hivi karibuni. Akiongea na
GOSPELGTV mjini Nairobi, Mchungaji Mmasi alisema kwamba serikali ina
mkono mrefu, lakini mkono huo unapotumika kuwanyamazisha wapinzani
kwa gharama yeyote, hapo ndipo serikali inapokosea. Aliitaka Serikali
ya CCM ijue kwamba mkono wa Mungu ni mrefu kuliko wa serikali. Habari
Zaidi
CCM
Wameanza kuua tena
Nchini
Tanzania Wanaopinga CCM chama kinachotawala kwa mabavu, Wanauawa.



Chuki
ambayo Serikali ya CCM inaipanda mioyoni mwa Watanzania, siku moja
watavuna matunda yake. Mkapa anamaliza muda wake vibaya. Asifikiri
wale anaowatesa akiwa madarakani, watamwacha aishi salama wakati atakapoachia
madaraka. Pesa alizowaibia Watanzania zitakuwa chungu kila senti.
Inashangaza Amerika wanamsakama Saddam Hussein na wanamwacha Mkapa
awaue Watanzania apendavyo. Mungu
atatulipizia kisasi.
Chuo Kikuu wasema 'NO' kwa CCM

(Picha
na Mroki Mroki)
Wanachuo wa Chuo Kikuu Dar es Salaam UDSM wakiandamana Dar kupinga
sera za Serikali ya CCM.Wanaitaka Serikali kupitia bodi ya udhamini
wa wanafunzi wa elimu ya juu HESBL, Kuwalipa haraka pesa zao za kujikimu.Walidai
hiyo ni haki yao na hawaoni sababu ya Serikali kutumia pesa za walipa
kodi kufanyia kampeni za CCM, huku wanafunzi na wananchi wakishindwa
kujikimu kimaisha.Walisema Tanzania siyo mali ya CCM na TRA, bali
ni ya Watanzania wote na wanachuo wakiwemo. Waliongeza kwamba hawaoni
sababu ya kuirudisha CCM madarakani ikiwa mbinu zao ni kuitumia TRA
kama silaha ya kuwatisha wananchi ili iwaibie mali zao. Walisema kwamba
wanafunzi na wananchi wamekondeana kwa njaa, huku viongozi wa CCM
na wafanyikazi wa TRA wakivimbisha matumbo kwa pesa za umma. Walionya
kwamba wizi huu wa mchana lazima ukome. Habari
Zaidi
Meet
The Kioko's
Bwana anapofanya kazi tofauti na mkewe, lakini bado wanakuwa na lengo
moja. Habari
Zaidi
Hakuna
Uchaguzi Tanzania bila Katiba mpya

Mchungaji
Faustin Munishi amesema hakuna Uchaguzi Tanzania bila Katiba mpya.
Akiongea katika Gospel GTV Pastor Munishi alivitaka vyama vya upinzani
Tanzania kuususia uchaguzi kwani CCM wakitumia katiba ya sasa wameumaliza
upinzani Tanzania. Kwa sasa ni sawa na hakuna upinzani. Kuingia kwenye
uchaguzi ambao CCM hawaruhusu wengine waseme, ni sawa na kuwafunga
vifaranga wa kuku na kuwashindanisha na mwewe. Matokeo mnayajua. CCM
wanajua walichofanya Tanzania kwa miaka zaidi ya arobaini, ndiyo maana
wananunua kila mtu. Pesa zilizo haki ya mikoa kimaendeleo, zinatumika
kuinunua mikoa iiunge mkono CCM. Alisema lazima Katiba ibadilishwe
kuwaruhusu wagombea binafsi ndipo upinzani wa kweli utakapoonekana
Tanzania. Alielezea nia yake ya kugombea Urais Tanzania bila chama
cha kisiasa. Mchungaji Munishi alisisitiza kwamba "Siasa ni uongo
na hawezi kujiunga na uongo ili awatoe waongo." Alisema kwamba
endapo CCM watakaidi kuibadili Katiba, basi wafuasi wake watamtangaza
rasmi kuwa Rais wa Gospel Tanzania. Kwa mara ya kwanza Tanzania
itakuwa na marais zaidi ya kumi. Huko ndiko tunakoelekea ikiwa CCM
watawaburuza watanzania kwenye uchaguzi bila KATIBA mpya. Habari
Zaidi

Munishi
awasili Tanzania

Mwinjilisti
na mwimbaji wa Nyimbo za injili Faustin Munishi yuko nchini Tanzania.
Aliwasili Mjini Arusha tarehe 4/10/05 kwenye basi la kampuni ya Scandinavia.Anatazamiwa
kutua Dar es salaam ambako atatangaza msimamo wake kuhusu uchaguzi
mkuu unaotarajiwa kufanywa mwezi huu. Awali Mchungaji Munishi aliwahi
kuviambia vyombo vya habari kwamba yeye anapinga uchaguzi Tanzania
bila katiba mpya.Alisema kwamba katiba ya sasa ina ujanja mwingi wa
kuirudisha madarakani CCM kiulaini. Alielezea masikitiko yake kwamba
upinzani Tanzania umemalizwa nguvu kwa hila za CCM wakiitumia katiba
ambayo Nyerere aliigeuza ilinde maslahi ya CCM hata kama yeye ni marehemu.Kwamba
msimamo wake bado ni huo, hiyo itajulikana atakapowasili Dar.
CCM sasa ni 'Mzoga'

Yalianzia viwanja vya KARIMJEE Dar es Salaam, na kumalizikia
Mnazi Mmoja. Yalikumba wa kila rika.Walisema ni maandamano ya kuchangia
watoto yatima, Lakini ujumbe kutoka mioyoni mwao ni kwamba CCM
OUT.Watanzania wengi wamechoshwa na KERO za CCM. Woga unawafanya
waseme wasiyomaanisha.Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. CCM
ni Nyani ambaye siku ya kufa kwake imefika. Haijalishi ujuzi wa miaka
arobaini kuparamia miti, Lakini safari hii miti yote inateleza. Watapigiza
chini kwa kishindo, na ndio mwisho wao. Watanzania tunataka ENZI MPYA
bila CCM. Habari
Zaidi


Kimurgor
Ameuawa



Aliyekuwa Mlinzi mkuu wa Moi Bwana Kimurgor,
ameuawa mjini Nairobi. Commando aliyesomea Israel, pia aliwahi kuwa
mkuu wa kikosi cha GSU wakati wa utawala wa Rais mstaafu Moi. Wakati
serikali ya Kibaki ilipochukua madaraka, Bwana Kimurgor alistaafishwa
na kuwa raia wa kawaida. Mpaka siku ya kufa kwake, alikuwa ofisa ulinzi
katika kampuni binafsi ya ndege. Inasemekana kwamba alikuwa akiendesha
mwenyewe ndani ya gari yake aina ya TOYOTA PRADO katika mtaa wa Fedha
Estate, alipokutana na watu watatu wenye silaha.Aliposimamishwa na
watu hao, alihisi hatari na kukaidi amri yao. Aliendesha kasi kuwapita
lakini commando safari hii hakuwa na bahati kwani walimfyatulia risasi
zilizoyakatiza maisha yake papo hapo.Polisi wameanza msako mkali,
huku vyombo vya habari vikiripoti kwamba wauaji wake walikuwa majambazi
wa kawaida. Ila hakuna chochote kilichoibiwa kutoka kwa marehemu.
Hata silaha yake aina ya pisto ilikutwa ikiwa sawa na risasi kumi
na moja ndani yake, jambo linaloonyesha kwamba commando hakuweza kuitumia
silaha yake kujikinga na watu waliopania kumuua. Habari
Zaidi
Mkurugenzi
wa EATV afariki
Je
alitolewa sadaka kwa Shetani?
Web Site ya Gospel kusheherekea machungu ya wengine?

Mkurugenzi mtendaji wa East africa TV na Redio bwana
Rodney Mutie Mengi amefariki mjini Dar es salaam Oktober 6 2005. Bwana
Mengi mwenye umri wa miaka 31, atakumbukwa na wapenzi wa muziki katika
EATV. Akiwa mkurugenzi, EATV pamoja na redio yake ilishika kasi katika
miji mikuu ya mataifa ya Afrika ya Mashariki. TV hiyo ambayo imekuwa
maarufu kwa kuonyesha miziki ya kidunia inayotukuza ngono na ufahari,
ilikuwa kero kwa waumini wa dini. Haikujulikana mara moja kilichosababisha
kifo chake, ila Taarifa tuliyoipata kutoka gazeti la NIPASHE, ilimkariri
baba wa Marehemu ambaye pia ni mmiliki wa utitiri wa vyombo vya habari
akisema kwamba mwanawe ameiaga dunia. Tangu kifo chake, Vyombo vya
habari vinavyomilikiwa na Mengi baba wa Marehemu, vimekuwa vikiripoti
watu mashuhuri waliofika kutoa rambirambi zao badala ya kuelezea kilichosababisha
kifo cha Mkurugenzi huyo. Tayari kuna uvumi mitaani, lakini GOSPELGTV
inawaomba wanaoeneza uvumi waache. Wakati huu wa majonzi utumike kuwapa
pole jamaa na marafiki wa marehemu, ili kama EATV itampata mkurugenzi
mpya, asikie kilio cha wengi kwamba TV hiyo inaupotosha umma kwa miziki
yao inayotukuza picha za ngono. Ikiwezekana wazipatie nyimbo za GOSPEL
kipau mbele na Mungu atawabariki. Hata hivyo GOSPELGTV tunawapa pole
jamaa na marafiki wa marehemu. Mungu anajua pa kuiweka Roho ya Marehemu.
Maombi yetu hayatabadilisha hilo.Habari
Zaidi

Rufftone wapambana na Ringtone
Walipotangaza vita magazeti yote
yaliandika. Sasa wanadai kupatana, magazeti yote kimyaaaa!!


Rufftone
wakiwa na Ringtone Kisii


Roy Smith Mwatia na Alex Apoko
Ni MARAPA wa Gospel. Usijali majina yao
ya Kiluhia na Kikamba, Lakini wanajulikana kama Rafftone na Ringtone.Kila
mmoja anadai kumzidi mwenzake katika kurap Gospel.Wanachosahau ni
kwamba wote ni mapandikizi ya vyombo vya habari. Siku Media itawaweka
chini, Huo utakuwa mwanzo wa mwisho wao.Pengine wajikaze kiusanii
wakite mizizi yao wenyewe. Lakini kwa mtindo huu wa kujiona wamefika,
tena mbaya zaidi wanajilinganisha na wasanii wa nchi za magaribi wakati
unga wa ugali kumudu ni shida,Tunasubiri tuone. Habari
Zaidi
'Arusha
Times' waiba story ya 'Nation'
Kumbe magazeti huibiana habari?
Ajabu ni kwamba STORY iliandikwa kwanza na Daily NATION, na badala
AT waseme waliikopi kutoka Nation, wao wanajifanya kwamba story ni
yao, tena wanadai imeandikwa na Staff Reporter wao.Waandishi wa habari
wanapoibiana habari, nini hawawezi kuiba? Gazeti la waswahili wanaoandika
kiingereza, siyo ajabu wakiamua kuwa majambazi wanaoiba story zilizoandikwa
kwa kiingereza sanifu.Kama kizungu kinawapiga chenga, si wawasiliane
kwa lugha wanayoijua kuliko kuamua kuwa majambazi wa habari? More

Mark
Kariuki alivyowatapeli Wachungaji Nairobi

Juanita Bynum akiwa na mwenyeji wake Mark Kariuki
Baada ya Mkutano uliofurika watu wengi Uhuru Park, Sasa Wachungaji
wanalalamika kwamba Mark Kariuki aliwatapeli.Aliwaita kwenye moja
ya Hoteli kubwa Nairobi, na kuwalisha chakula cha jioni. Kisha aliwauzia
sera zake kuhusu mgeni anaetarajia kumwalika. Aliwataka wachungaji
hao kuchangia mkutano huo kipesa kwani angetaka kuwaonyesha Wamarekani
kwamba Afrika wanaweza kuudhamini mkutano wa Injili.Wachungaji walikubaliana
naye na kuanza kuuchangia mkutano. Ilipofika siku yapili ya Mkutano,
wachungaji hawakuyaamini masikio yao pale mgeni wao alipotamka kwamba
alituma shilingi milioni nane kuugharamia mkutano huo.Kwa sasa vidole
vyote vinaelekezwa kwa Mark Kariuki pamoja na Kanisa la Deliverence
Church waliouteka mkutano huo. Umoja bandia, sasa umeishia kulaumiana.
Habari
Zaidi
Serikali
Yajikanyaga

Polisi
mjini Nairobi wakionyesha vifaa vipya ambavyo Serikali iliagiza kutoka
ngambo ili kuwanasa madereva walevi. Wenyewe Serikali
wameruhusu pombe ziuzwe kila mahali, na sasa wanawasaka madereva walevi.
Je itakuwa kuwanasa madereva walevi, au ni kuwaambukiza magonjwa kutumia
vyombo hivyo ambavyo vinatumiwa na Polisi wasiozingatia masharti ya
afya? Wanaotumia vyombo hivyo, hulazimishwa kupuliza ili kiwango cha
pombe miilini mwao kijulikane?
huku
wengine wakiacha mate yao mahali ambapo lazima kila dereva aweke mdomo
wake hapo.
Je hiyo
ni sawa?
Pirater Mkuu Anaswa

Mwenye koti jekundu ni Mwandishi wa Habari akiwategea sikio wasanii
nje ya makao makuu ya Nation Media. Kilio chao ni wizi wa kazi zao.
Walidai kwamba wamemnasa mshukiwa ambaye wanadai ndiye mzizi mkubwa
wa wizi wa kazi zao za kisanii. Habari
Zaidi
Tanzania wabadili
pasipoti tena
A country without National IDs, but they keep on changing passports
every now and then.
What a SHAME?



Mchungaji Munishi akiwa katika ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini
Nairobi hivi majuzi. Alikuwepo kuibadili pasipoti yake, kufuatia zoezi
la serikali ya Tanzania kuzibadili hati za kusafiria.
Wenye pasi wanatakiwa kuomba upya, na kutimiza masharti yote ikiwa
ni pamoja na kulipa shilingi elfu nne za Kenya. Isitoshe kila mwombaji
lazima achukuliwe alama za vidole vya mikono yote miwili. Wadadisi
wa mambo ya kisiasa wanahoji uhalali wa serikali kubadili pasipoti
wakati huu wa uchaguzi. Wengine wanaliona hilo kama mbinu ya serikali
ya CCM kutafuta pesa za kuugharamia uchaguzi. Pasipoti ambayo ilikuwa
ikigharimu shilingi elfu tano za Tanzania, sasa inagharimu zaidi ya
shilingi elfu hamsini za Tanzania. Je mwananchi wa kawaida Tanzania
atapata wapi TSHS.50,000? Habari
Zaidi
Eti Wanjiru Kahaba?




"BIshop" Magreth Wanjiru Ametangaza rasmi kutounga mkono
katiba mpya ambayo Kibaki anataka wakenya waipitishe kwenye kura ya
maoni. Magazeti nchini Kenya yameanza kumchambua Mama Magreth Wanjiru
huku mengine yakimwita Kahaba. Je kuna ukweli kwenye tuhuma hizo?Habari
Zaidi
Gospel
Television Moto wa kuotea mbali
Ikiwa ndio kwanza inajitayarisha kurusha
matangazo yake, GTV imekuwa tishio kwa Serikali Tanzania. Aliyekuwa
Rais wa kimabavu nchini humo William Benjamin Mkapa aliamuru polisi
wawatie mbaroni wote watakaopatikana na VCD za GTV. Kisa ni kwamba
Gospel Television ilikuwa imezungumzia uwezekano wa Mkapa kukamatwa
na kufunguliwa mashtaka kwa kutumia madaraka vibaya. GTV ilikuwa imedai
kwamba, Mkapa akiwa madarakani aliwaamuru POLISI wawaue Wazanzibari
zaidi ya 70 kwa kosa la kusema CCM Chama Cha Majambazi hawakitaki.
Pamoja na mambo mengine GTV ilipendekeza tume ya kumchunguza Mkapa
iundwe na akipatikana na makosa sheria ichukue mkondo wake. Pia GTV
ilidai kwamba Mkapa aliitawala Tanzania kama mali yake binafsi kwani
hakutaka ushauri wa mtu yeyote. Bado msimamo wa GTV ni huo na hatuombi
msamaha kwa Mkapa wala CCM. Habari
Zaidi
Hotuba
ya Munishi kwa TAIFA 
Vs


NTV
Wavuta viatu badala ya Soksi
Kuboresha NTV Haimaanishi kupora watangazaji kutoka KTN. Badala
yake inaonyesha uvivu wa kutengeneza watangazaji wenu, au kuwatafuta
wapya.
Baada ya kurupushani na Lucy, sasa Nation wanaonekana kushika adabu.
TV yao wanasema itatuwasha badala ya sisi kuiwasha.Wengi wametafsiri
hiyo kama ongezeko la vipindi vinavyohusiana na "ngono"
Tayari wameanza kuonyesha nyimbo ambazo waimbaji na wachezaji wako
nusu uchi kama siyo uchi kabisa. Ikiwa walimaanisha kuiwasha jamii
kwa jinsi hiyo, basi wamekosea. Tunatakiwa kulaani vipindi vya ngono
kwenye TV. Na Nation wajue hivyo..Habari
Zaidi
GOSPELTV WATCH PRO-LIFE VIDEOS
GTV
Online
Gospel Television ambayo Studio zake ziko Nairobi Kenya, Sasa itaanza
kurusha matangazo yake kutumia Internet. Mipango yote imekamilika
na tuko mbioni kukamilisha ile ya kiufundi ili tuwe Online ulimwenguni
kote. Endelea kuutupia macho ukurasa huu. Kwa sasa unaweza kuisikia
sauti ya GTV. Habari
zaidi
Gospel
Redio FM
Sasa unaweza kuisikiliza
Redio INJILI FM OnLine.
TAHARIRI:
Wahubiri Tegemeeni Mungu 
Wimbo
mpya "Nateseka Natukuza"

"Wanahabari
Wanafiki" Wimbo 
MASAI: "Hakuna
Nuru Gizani" VICHEKESHO
Hotuba ya Munishi
kwa TAIFA 
"Yesu atakuponya
bure" TAHARIRI
Wimbo mpya "Mpende
Adui "
GUMZO"Aibu
wanahabari!! "

Habari za hapa na pale

Kenedy
Ochieng Asema ana UKIMWI Mugabe
na Mkapa lao moja
Gospel
tape banned by Dar officials Vituko
Makanisani Sokoni
Gikomba
Munishi
Magazetini
Hotuba
ya Munishi kwa TAIFA

Kisii
yaongoza kwa Injili

















Wachungaji na wageni walioudhuria kongamano la kipekee mjini kisii.
Habari
zaidi
Tuzo la Mwanzo wa Mwisho?
Ester Wahome Mwimbaji
wa nyimbo za Injili akipokea tuzo la KISIMA kutoka kampuni ya "Nation"
Pamoja nae ni mwimbaji wa nyimbo za dansi Saimoni Kihara maarufu kwa
jina la Musaimo. Kwamba makanisa yamewatupa waimbaji wao mpaka kufikia
hatua ya kupewa tuzo na watu wasio wa Kanisa tena kwenye vilabu vya
usiku, hiyo ni aibu kwa Kanisa pamoja na waimbaji wanaokubali kuidhalilisha
Injili. Tuzo la waimbaji wa Injili liko mbinguni. Lakini haya matuzo
ya kina "Nation" na mengine ya watu 'Wa Kora", yanawafaa
wenyewe. Ndio maana kila mwimbaji wa Injili aliyekubali kupewa tuzo
za kidunia, inakuwa huo ndio mwanzo wa mwisho wake. Tunaomba mambo
yasiwe hivyo kwa Ester Wahome. Habari
Zaidi




50 wafa Ukambani Baada ya kunywa
pombe ya sumu








Hawa ni baadhi ya waasiriwa wa pombe hiyo ambayo Serikali inaiita
haramu
Takriban watu 50 wamepoteza
maisha yao baada ya kunywa pombe inayosadikiwa ilikuwa na kemikali
za sumu. Pombe hiyo maarufu kama 'KUMI KUMI' huuzwa shilingi kumi
za Kenya. Watu wengi wa kipato cha chini wamekuwa hawana jinsi isipokuwa
kuibugia 'KUMI KUMI' baada ya kazi ngumu mchana. Tukio hilo la kushangaza
lilitokea Machakos kilomita 50 kutoka jijini Nairobi.Kufuatia tukio
hilo Rais Kibaki ameamuru Polisi wasake pombe zote za kienyeji nchi
nzima Habari
Zaidi
Ajali
ya Kutisha
Moja kati ya ajali mbaya Tanzania
HABARI
ZAIDI
Gazeti
la "MWANANCHI" Tanzania lafichua
Tizama
video ya Munishi
Umewahi kujiuliza
kwa nini mabalozi wa Tanzania nchi za nje karibu wote ni wanajeshi
wastaafu? Je Serikali huwatumia kufanya ukachero kwenye nchi hizo?
Au hujihusisha na mambo ya kidiplomasia kama yalivyo? Je wanajeshi
na wanadiplomasia ni taaluma moja? Kwa nini Serikali zote tangu Nyerere
zimekuwa zikifuata desturi hiyo? Je ni mbinu ya kuwatawanya wanajeshi
ili wasiweke vichwa pamoja kuitoa serikali dhalimu ya CCM? Hayo na
mengine mengi, Mwandishi wetu atayaangalia katika makala haya.
Habari zaidi
"Standard"
Kenya Latoboa siri
Aibu
Yaifunika Tanzania







Serikali ya Mkapa imefanya kosa la kiistoria pale ilipowafukuza waandishi
wa habari wa nchi jirani ya Kenya. Waliyataka wenyewe, na yalipokuja
sasa wanayakimbia. Baada ya gazeti la "Mwananchi' kuuzwa kwa
kampuni ya 'NATION", Wakenya waliwekeza mabilioni ya dola za
Kimarekani katika sekta ya habari na utangazaji nchini Tanzania. Kile
ambacho hawakukijua, ni kwamba sekta hiyo haijawahi kuwa huru Tanzania.
Walipoanza kuandika habari kulingana na taaluma yao, gazeti la 'Mwananchi'
lilianza kuchanja mbuga Tanzania, na kuwa moja kati ya magazeti yanayoongoza
nchini humo. Serikali ikaliona hilo. Kama kawaida yao kuthibiti habari,
walijaribu kulitumia gazeti la 'Mwananchi" liwapigie debe CCM
wakati huu wa uchaguzi. Inasemekana wanataaluma hao waliikatalia serikali
usoni, jambo lililosababisha kutimuliwa kwao. Mkapa ameithihirishia
dunia kile ambacho walikuwa wakikijua tayari. Kwamba Tanzania hakuna
uhuru wa kutoa mawazo. Na kwamba utitiri wa vyombo vya habari Tanzania
ni kifunga macho ili jumuia ya kimataifa ione kwamba kuna uhuru wa
habari, kumbe asilimia 99 ya vyombo hivyo humilikiwa na serikali pamoja
na maajenti wake. Inasemekana Mkapa mwenyewe anamiliki zaidi ya magazeti
8 yakiwemo yale ya kidini ambayo hayaachi kuweka picha yake mbele.
Anapomaliza urais na kuirudia kazi yake ya uandishi, Mkapa atakumbukwa
kama mwanahabari aliyepata madaraka yakamlevya, kisha akaanza kuwatesa
wanahabri wenzake.

Serkali ya Tanzania inaongozwa na wahuni. Usipounga mkono maovu yao,
basi watakufanya chochote. Watatumia kila chombo cha dola. Idara ya
UHAMIAJI ikiwa mojawapo. Ni kawaida yao. Wamezoea. Na hawapelekwi
kokote. Kinachoniumiza moyo, ni mabilioni ya shilingi za Kenya "NATION
walizotapeliwa na Serikali ya Tanzania. Kwamba sasa wanawatimua, Mtu
anaweza jiuliza kwa nini waliwauzia kampuni hiyo ya "MANANCHI"
ikiwa kuwapa vibali ni vigumu? Hata kama wewe ni Mtanzania usishangae
kuitwa mkimbizi kutoka Zambia. Wana habari wa "NATION" wako
Tanzania kufanya kazi kulingana na taaluma yao na siyo kuipigia debe
CCM. Kama Mkapa alifikiri kwamba "NATION" ni "UHURU"
na "MZALENDO" magazeti ya chama, atakiona kilichomnyima
kuku kutoa maziwa anyonyeshe vifaranga. Namshukuru Mungu kwamba "NATION"
wamejionea wenyewe yale ambayo nimekuwa nikiyalalamikia kwa miaka
mingi. Kanda yangu ilipigwa marufuku kwa kusema "CCM aliyoanzisha
Nyerere imezeeka, Sijui "MWANANCHI" walisema nini. Lakini
Wahuni wa DAR, wameanza fujo zao. Safari hii wameuma kubwa kuliko
uwezo wao kutafuna. Pengine wateme. Wakimeza itawakwama kooni.Jipeni
moyo "NATION" Mungu ni mkuu kuliko CCM na Mkapa mwanahabari
anaewatesa wanahabari..Habari
Zaidi




Zanzibar
Kunaashiria Moto
Pastor
Pius Kongo Alaumiwa




Pastor Pius Kongo Aliyekuwa TAG Moshi mjini, kabla ya kufungua
kanisa lake. Ambalo sasa linamtupia kila aina ya lawama Habari
Zaidi
Jihadhari
nao ni WASHIAMA!!


Washiama
Vijana mashuhuri wa kuimba nyimbo za Injili nchini Kenya Habari
Zaidi

Waislamu
wamlalamikia Mwinyi


Aliyekuwa Rais wa awamu ya pili Tanzania Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi
Watanzania wanamheshimu kwani yeye ni nyota ya mabadiliko Tanzania.
Alikuwa na ujasiri wa kupinga sera za Nyerere akiwa hai, na kuleta
mageuzi Tanzania ambayo Mkapa ameyadidimiza matumaini ya Watanzania.
Habari
Zaidi
"Kikwete
Tosha" asema Mchungaji

Mchungaji Paul M.K. Mduma Akiwa katika Ofisi za GTV alielezea masikitiko
yake kwamba, vyombo vya habari vimeanza kumchafua Kikwete aliyemjua
tangu akiwa mwanafunzi Kibaha Secondary School. Alidai kwamba walisoma
wote kwa muda wa miaka minne. Tangu mwaka 1966 hadi 1969 Habari
Zaidi

Waruinge
Atawazwa Uchungaji


Alikuwa kiongozi wa kundi la Mungiki ambalo Serikali ya Kenya ililiita
"kundi haramu" Aliokoka mwaka 2003 na miaka miwili
baadaye alitawazwa kuwa Mchungaji Hezekia Ndura Waruinge
Kikosi
cha Living Water Kawe
Waimbaji wa kikundi cha Living Water wakiimba nyimbo za kumtukuza
Mungu

Komba
Ajikomba na CCM



Wanamwita "Kapteni" Komba Msanii anayetumia sanaa yake kuwatukuza
wanadamu badala ya Mungu. Sasa anajuta kuwapandisha wanasiasa ngazi
huku mwenyewe akibaki chini.Anasema kama siyo yeye Mkapa asingeuona
Urais na hatimaye awe tajiri wa kutisha Tanzania. Mkapa alimsahau
Komba mara tu alipoingia Ikulu. Mungu anamwita Komba amtumikie. Uzee
unapomnyemelea Komba, laiti angeona mwanga amtukuze Mungu badala ya
wanasiasa waongo.Kila la Kheri Bwana Komba.
Padre
Atuhumiwa kwa UBASHA

Padre Sixtus Kimaro Akiwa mahakamani Kisutu Dar.
Ameshitakiwa kwa tuhuma za kumlawiti mvulana wa miaka 17
Sisi tunasema "Lisemwalo Haliko, Kama liko, Lilikuwepo."
HABARI
ZAIDI
Simbeye
Mchawi Aliyeokoka




Bwana Zebius Mulingwa Simbeye
Akiwa na Joyce Wairimu Maina Kericho Kenya

Mtoto
apatapo Mtoto




Siri za Kakobe

Askofu Nnko
ailalamikia Serikali
Kuishi
Amerika ni haki yako
Samples. 6 second of every song


 |
SIDE A
- Yesu Aliniita
- Bwana Nashangaa
- Tuonane Milele
- Wamwendea Yesu
- Msalabani Pa Mwokozi
- Yesu Kwetu Ni Rafiki
|
SIDE B
- Bwana Uliyewaita
- Kumtegemea Mwokozi
- Sioni Haya Kwa Bwana
- Yesu Unipendae
- Yesu Nakupenda
- Ati Tuonane Mtoni
|


Twende
nikutembeze Nairobi





